Mayweather78
Member
- Jul 20, 2017
- 45
- 142
Salaam,
Napenda kuchukua fursa hii kuwapa elimu kwenu wamiliki wa makampuni (wasimamizi wake) na wasiomiliki kampuni kwa maana biashara Local au wasimamizi wa ajira zisizo rasmi hasa linapokuja Suala la UAJIRI.
Kitendo cha kumuajiri mfanyakazi kinakwenda sambamba na mambo yafuatayo:
1. Mwajiri tambua kuajiri mfanyakazi sio kama unamsaidia (mnabadilishana huduma kwa fedha)
2. Mwaniri tambua Mshahara ni haki ya kila mfanyakazi aliyetimiza wajibu wake sio OMBI
3. Mwajiri ONDOA Masharti yasiyotekelezeka ambayo wafanyakazi wanalazimika kufanya ili kujinasua tu na Adui UMASIKINI ila anakulaani kila siku kwa MUNGU subiri ANGUKO lako.
4. Mwajiri huyo Mfanyakazi unayemuona sio wa thamani kwako ila nyumbani kwake ni baba, mama, kaka, dada au shangazi anayetekeleza majukumu yake kupitia jasho analolitiririsha kwenye kazi zako.
5. Mwajiri Mafanikio yako yanategemea uwepo wa wafanyakazi walioamua kutekeleza majukumu yao pengine nje kabisa ya yaliyomo kwenye maelezo ya kazi (Job description)
6. Mwajiri usiamini kuwa mfanyakazi wako ana shida ndyo maana anafanya kazi kwako HAPANA ni muda ndyo umeamua awepo hapo
7. Mwajiri usimtishie mfanyakazi wako kumfukuza KAZI kila anapokosea tambua UNAUA vitu vingi sana moyoni mwa mfanyakazi wako mwenyewe.
8. Mwajiri usitangaze makosa na matatizo ya mfanyakazi kwa wengine maana unatengeneza BOMU eneo lako la kazi
9. Mwajiri jiepushe na UPENDELEO wa aina yoyote ili kutengeneza usawa mahala pa kazi.
10. Mwajiri tambua UKALI sio LUGHA ya uendeshaji wa kazi zako, unaweza kuweka system na programs nzuri ambazo zinatekelezeka bila hata kutumia nguvu kubwa kugombeza wafanyakazi.
Natumaini Nimeeleweka.
Wabillah Tawfiq