Elimu Ya Fedha ni Hitaji la Leo

Elimu Ya Fedha ni Hitaji la Leo

Joined
Apr 5, 2024
Posts
81
Reaction score
117
Habari wanajamvi,
Nimerudi tena baada ya kufika Morogoro salama. Treni iliondoka kwa wakati (saa 12:55) na kufika kwa wakati (saa 2:59). Nilichukua bajaji ya elfu 2, nikafika Msamvu nlikoacha pikipiki. Nikawasha chombo, nikajaza mafuta, nikafika home salama.

Nimekuwa na tabia ya kusoma kurasa 10 za kitabu fulani asubuhi. Nina shauku sana ya kufikia malengo makubwa ya kifedha, nitaanza na elimu ya uchumi (ambayo na mimi ilinisumbua kwa muda mrefu).

Mwaka jana, nilinunua kitabu kinaituwa FINANCIAL INTELLIGENCE (AKILI YA UCHUMI) ilo andikwa na KAREN BERMAN pamoja na JOE KNIGHT.

View attachment 3217423

Nilianza kusoma kitabu hicho na kimenibariki sana. Kuna vitu vingi sana katika kurasa za awali. Lakini kilichonigusa sana ni CASH FLOW na PROFITS.

Nilikuja kufahamu kuwa watu wengi sana sana (haijalishi kuwa amesoma au hajasoma. Hata wafanyabiashara wengi wanajikuta hapa), hawajuagi tofauti kati ya maneno haya mawili. Naomba kutumia dakika chache kuelezea.

PROFITS (FAIDA)
Profits au faida ni pesa unayoipata kwa kazi uliyofanya, baada ya kuondoa matumizi yote. Kwa mfano, ukinunua tikiti ya sh 10,000 sokoni ukatengeneza juice ya 50,000, unapata faida ya 40,000. Hii huwa the case biashara inapokuwa katika eneo moja, na una walk-in customers (wateja na kuja na kuondoka, wanaolipa fedha taslimu).

Biashara yako inapokua, unalazimika kufikiria tofauti kuhusu faida. Utakutana na wakopaji. Kwa mfano, hoteli fulani inaweza kupenda kazi yako, wakakupa tenda ya kutengeneza juice ya sh. 500,000. Utajitutumua na kutafuta tikiti ya sh. 100,000, kisha ukatengeneza na kupeleka. Faida ya 400,000, au siyo?!

Lakini je, faida hii inamaanisha una hela mkononi? Hapa ndipo suala la cash flow linapoingia.

CASH FLOW (HELA INAYOZUNGUKA)
Cash flow ni pesa ulizofanyia kazi kukufikia mkononi kwa ajili ya matumizi. Tukirejea mfano wa hapo juu, ushapeleka chakula, washakula na kusaza, umeokota makombo, na baadaye mmekaa na bosi kupiga mahesabu. Unadai LAKI 5 zako. Unaombwa uandike invoice. Unafanya hivyo. Jumatatu asubuhi na mapema, imo.

Hapo, una cash flow.

UMUHIMU WA FAIDA NA CASH FLOW
  • Faida huwa ni kipimo cha kuashiria kama biashara yako inafaa. Bila faida, biashara yako haiwezi kustahimili mwendo mrefu.
  • Cash Flow (Pesa Mkononi) hukusaidia kuhandle matumizi vizuri na mapema. Biashara inaweza kuwa na faida, lakini ikashindwa kulipa bili zote kwa wakati.
CASH FLOW IS KING.
Ni muhimu kuwa na pesa mkononi. Hili ni suala linalowasumbua wafanyabiashara wengi, hasa wadogo, au wale wanaoanza.

Nimesikia vilio vingi vya ulaji wa mtaji mtaani kwetu. Uchunguzi ukaonyesha kuwa alikuwa afahamu tofauti kati ya faida na pesa mkononi.

Tafiti zinaonyesha kuwa zaidi ya 80% ya biashara ndogo hufilisika si kwa sababu ya kukosa faida, bali kwa sababu ya ukosefu wa cash flow.

Ili kukabiliana na changamoto za "pesa zisizoonekana", mfanyabiashara mdogo anaweza:
  • Kuwasiliana mapema na wateja kuhusu malipo
  • Kutumia mikataba iliyo na masharti ya malipo ya haraka
  • Kuwa na akiba ya dharura ya kifedha
Ni muhimu kupanga mikakati ya kuongeza faida, kudhibiti matumizi, na kuhakikisha unakuwa na fedha taslimu kwa dharura na matumizi ya kila siku, yasiyosubiri.

Na maneno haya sio kwa wafanyabiashara tu. Nazungumza nawe mwajiriwa, mwanafunzi, na bachela. Ni muhimu kuwa na hela mkononi kwa ajili ya dharura. Na matumizi. Na umeme, na kodi ya nyumba.

Niishie hapo. Siku nikipata muda, nitazungumzia THE SEVEN BABY STEPS TO ECONOMIC FREEDOM (Hatua 7 rahisi za kujipatia uhuru wa kiuchumi).

Hadi tutakapokutana tena, alamsiki...
 
Kuna tofauti kati ya:

FINANCIAL EDUCATION
FINANCIAL LITERACY
FINANCIAL INTELLIGENCE

Shule wanafundisha hyo ya kwanza ambayo haina msaada wowote mtaani ila hizo mbili inabidi uchimbe sana ndio maana kitabu kimeitwa financial intelligence and not otherwise.

Ukisoma hicho kitabu kinaelezea kwamba company nyingi zinafilisika kwasababu ya kukosa financial intelligence yaani watu wanaangalia hesabu za uongo za kwenye computer zilizopikwa na wahasibu wakati uhalisia sio huo.

One of the best book I have ever read on financial issues.
 
Pia kuna Asset na liability watu wengi wakipata pesa wananunua liability wakijitutumua na kununua asset basi watalazimisha kupiga mahesabu makali eti eka itarudi? Mimi nasema afadhali uwe na biashara au asset yenye faufaida kiduchu kulikokununua liability.
By the way huyo attachment haifunguki ni.nini uliatach au hicho kitabu?
 
Kuna tofauti kati ya:

FINANCIAL EDUCATION
FINANCIAL LITERACY
FINANCIAL INTELLIGENCE

Shule wanafundisha hyo ya kwanza ambayo haina msaada wowote mtaani ila hizo mbili inabidi uchimbe sana ndio maana kitabu kimeitwa financial intelligence and not otherwise.

Ukisoma hicho kitabu kinaelezea kwamba company nyingi zinafilisika kwasababu ya kukosa financial intelligence yaani watu wanaangalia hesabu za uongo za kwenye computer zilizopikwa na wahasibu wakati uhalisia sio huo.

One of the best book I have ever read on financial issues.
Financia education ndio financial literacy.
 
Back
Top Bottom