Elimu ya jando na unyago

Elimu ya jando na unyago

chakochetu

Senior Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
108
Reaction score
35
ELIMU YA JANDO NA UNYAGO:
  1. Sio Elimu ya kuiga mambo ya Mila zingine[hakuna mapokeo ya mila nyingine],ili lenga jamii husika tu.
  2. Hakuna Cheti kinachotolewa,bali wote wanafaulu
  3. Kumbukumbu ya Elimu yako ni RIKA LAKO
  4. Kila mwanafunzi anajiamini
  5. Hakuna njia ya mkato katika kuipata Elimu ya jando na unyago[Hakuna wizi wa mtihani,hakuna kukariri]
  6. Elimu hii iliwaunganisha wanajamii katika ushirikiano wa shughuli mbalimbali za kijamii.!!!
  7. Muda wa kuipata Elimu ni mfupi.

Hebu angalia ELIMU YA CHETI :
  1. Elimu ya mapokeo,kutoka sehemu zingine,inakuwa na malengo mahususi.!!,Elimu za cheti zimewabadili watu kuwa tofauti na mila zao,na wamekuwa na kasumba ya mapokeo ya Mila zingine[Ukiwa Daktari,Basi Utamdharau aliyesoma kozi ya aina fulani.!!!]
  2. Cheti kinachotolewa,kipimo chako ni ufaulu katika daraja utakalo pata.
  3. Kumbukumbu ni Aina ya kozi uliyosomea.
  4. Mwanafunzi hawajiamini,mpaka matokeo yatoke,na ili kufaulu lazima urudie na kukariri mawazo ya mtu wa zamani tena wa mila tofauti(watunzi wa vitabu,wavumbuzi).Wengine wanaiba mtihani ili kufaulu.!!
  5. Elimu ya Cheti imewagawa watu;utafanya kazi kutokana aina ya kozi uliyosomea;utakuwa katika kundi fulani katika jamii kutokana na daraja ya cheti chako.!!!
  6. Watu wanatumia muda mwingi kuitafuta Elimu ya Cheti.

TOFAUTI TULIZO NAZO ZIMECHANGIWA NA ELIMU YA CHETI
!!!!!!!!,wala tusihusishe sababu zingine,eti tunanyoosheana vidole,mila zetu ziko wapi.?!!!,kila mtu anaheshimika kwa mila na utamaduni wake.>>>>

EXCEPTIONAL RULE:UNAWEZA KUFANIKWA BILA KUWA NA CHETI........(dunia ina maajabu.!!!)
 
Back
Top Bottom