Kuacha mambo yaende yatakavyo kama ndugu yangu anavyotaka kufanya "yangu macho" ni kutoitendea haki nchi hii! Sasa ikiwa kila mmoja wetu ataamua mambo yaende hivihivi itakuaje? Ni wajibu wetu kukemea tunapoona mambo hayaendi kama tulivyotarajia, na kuchukua hatua mahususi kila inapobidi.
Ndugu yangu thinker96 analalamika kua kuna mwalimu ukichelewa kukusanya assignment hakutambui! Mimi nadhani huyu mwalimu alipaswa kupongezwa! kwa nini usikusanye assignment kwa wakati. Tabia za uvivu na kuto meet deadline tangu tukiwa wanafunzi ndo zinasababisah hatuwezi ku meet deadline hata tunapokua kazini au tunapoendesha shughuli zetu binafsi! Matokeo yake miaka hamsini baada ya uhuru bado sisi ni maskini sana!
Ku-meet deadline ni muhimu sana katika maisha, uwe mwanafunzi, mfanyakazi na hata mkulima! Kwa mfano ukiwa mkulima na huwezi kulima na kupanda kwa wakati, nini matokeo yake? Hutapata mavuno! Hapa ninapoendesha shughuli zangu za ujasiriamali, am strict when it comes to deadline. Hii ni kwa sababu our survival depends on our customers' satisfaction. Tusipofanya hivyo wateja weatahamia kwa wachina halafu kama kawaida yetu tutabaki kulalama.