Kama ulikua hujui kuwa Duniani kuna mtu alitunga WIMBO uliopelekea watu zaidi ya 100 kufariki,
Akiwemo Yeye mwenyewe na aliekuwa mpenzi wake baada ya kuachwa na mpenzi wake huyo wacha nikufahamishe;-
Wimbo huo unaitwa Gloomy Sunday (Jumapili ya Huzuni),
Kama hujawahi kuusikiliza nenda kausikilize,
Natoa onyo kabisa Kama umeachwa usiusikilize huo wimbo utaibua maumivu makubwa katika moyo wako,
Na sio tu maumivu unaweza kupoteza maisha hata wewe,
Ni wimbo uliojaa hisia kali za kuachwa na ukikosa kujiua basi lazima ulie,
Ni wimbo wenye huzuni zaidi Duniani Kuliko wimbo wowote,
Ni wimbo uliotungwa na Rezso Seress a .k. a (Rudi Spitzer),
Ni msanii kutoka nchini Hungary mwaka 1933.
Reszo alitunga maneno ya wimbo huo na kupiga mwenyewe ala ya huzuni ya wimbo huo, baada ya kuachwa na mpenzi wake.
Inaelezwa kwamba kitendo cha kuachwa na mwanamke aliyekuwa akimpenda sana,
Kilimfanya apatwe na huzuni kali na msongo wa mawazo,
Na katika kipindi hicho ndipo alipopata wazo la kutunga mashairi na baadaye kuutengeneza wimbo huo.
Kwa sababu aliuimba akiwa na huzuni kali,
Wimbo nao ulijawa na hisia kali, za mtu anayelalamika kuvunjwa moyo na mpenzi wake,
Akifananisha kitendo cha kuachwa kuwa sawa na kufiwa na mpenzi aliyekuwa anampenda.
Awali ulionekana kuwa wimbo wa kawaida wa huzuni,
Lakini matukio ya watu kukatisha maisha yao baada ya kuusikiliza mara nyingi wimbo huo kwa kuurudiarudia yalianza kuripotiwa,
Wengine wakiacha kabisa ujumbe kwamba wamejiua baada ya kusikiliza wimbo huo,
Miaka miwili baadaye, serikali ya Hungary iliupiga marufuku wimbo huo,
Hata hivyo tayari ulikuwa umesambaa sana,
Kiasi kwamba watu bado waliendelea kuusikiliza,
Hasa pale inapotokea mtu ameachwa au ameumizwa na ampendaye.
Sifa za wimbo huo zilianza kusambaa duniani kote na mwaka 1936,
Wanamuziki wa Marekani na Uingereza waliutafsiri wimbo huo kwa lugha ya Kiingereza kutoka lugha ya awali ya Ki-hungary,
Bado tatizo lilelile likawa linaendelea hata kwa matoleo yaliyotafsiriwa,
Watu wakawa wanaendelea kujiua baada ya kuusikiliza.
Mwanzoni mwa miaka ya 1940, toleo la Kiingereza la wimbo huo lilipigwa marufuku nchini Uingereza,
Marufuku hiyo ilikuja baada ya idadi ya waliokuwa wakijiua kuzidi kuongezeka,
Lakini Marekani na sehemu nyingine duniani wimbo huo uliendelea kupigwa
Wimbo huo ulimfanya jamaa awemaarufu sana Duniani na kumpatia kipato kikubwa Cha Pesa,
Miaka michache baada ya wimbo huo kumpatia mafanikio makubwa na kuwa gumzo dunia nzima,
Seress aliamua kumtafuta mwanamke aliyemuacha na kusababisha atunge wimbo huo,
Lengo lake likiwa ni kujaribu kumbembeleza ili warudiane kwani kama ni pesa, tayari alikuwa nazo baada ya wimbo huo kuwa maarufu dunia nzima.
Hata hivyo, katika hali ya kustaajabisha Seress alipofika mahali alipokuwa akiishi mwanamke huyo,
Alikuta watu wamejaa baada ya kuuliza aliambiwa tupo kwenye msiba na aliekufa Ni huyo mwanamke,
Baada ya uchunguzi ikabainika kwamba mwanamke huyo alijiua kwa kunywa sumu,
Baada ya kufanya uchunguzi ndani ya Chumba alichojiua ilibainika kwamba alikuwa akisikiliza wimbo huo,
Ndani ya Chumba hicho pia aliacha ujumbe wenye maneno mawili, kama sababu za kujiua kwake,
Maneno hayo yalikua ni" Gloomy Sunday".
Baada ya tukio hilo Seress alibaki na hatia kubwa ndani ya moyo wake,
Akiamini kwamba yeye ndiyo chanzo cha kifo cha mwanamke huyo,
Ilipofika mwaka 1968, naye aliamua kuyakatisha maisha yake kwa kujirusha ghorofani kupitia dirisha la chumba alichokuwa akiishi, nchini Budapest.
Seress aliacha ujumbe kwamba ameamua kuyakatisha maisha yake baada ya kuona wimbo alioutunga,
Umekuwa sababu za watu wengi kujiua hivyo anahisi anahatia kubwa ndani ya moyo wake,
Lakini pia katika ujumbe huo alimaliza kwa kuwaomba radhi watu wote waliojiua kwa sababu ya kusikiliza wimbo huo.
Brother wanaoogopa kufa ni sisi waafrika tu ila wazungu na waarabu kufa kwao sio tatizo,
Ndio maana wenzetu wameendelea Sana.
Makala hii imeletwa kwenu na Dhulkad Madara Morogoro.