Elimu ya majirani ndio inakwamisha EAC

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
EAC ina kila kitu na kila sababu za kupaa na kuwa ukanda bora Afrika, lakini mojawapo wa sababu zinazofanya tukwame ni elimu duni ya baadhi ya majirani zetu kwenye huu muungano. Na hii imechangia sana kuona watu wana kauli za kiajabu hata huku Jamii Forums.

Mfano hai, majirani zetu Tanzania, unakuta mwanafunzi anafikia hadi darasa la saba halafu anafanya mtihani wa mwisho wakati hajui kusoma wala kuandika. Haingii akilini, yaani afikie hadi kwenye mtihani wa mwisho akiwa kilaza bila uwezo wa kusoma wala kuandika. Halafu wanaachiwa na kuingia sekondari/upili na kuendelea, hatimaye ndio hawa wanapata simu baadaye na kuingia kwenye mitandao ya kijamii na kutuzingua kila siku.

Kweli ni hatari, maana eti ndio kizazi kinachotegemewa kuhusika katika ushirikiano wa kesho baina ya nchi zetu hizi. Hapo unakuta watu wananuna kwa kila azimio, kumbe tatizo ni elimu. Juzi wametutukana sana baada ya kusikia watoto wetu wa darasa la kwanza wanapata laptops.

Taarifa kamili hii hapa


Wanafunzi wasiojua Kusoma na Kuandika wanafaulu vipi Mtihani wa Darasa la Saba? | Fikra Pevu

KILA mwaka zimekuwa zikitolewa takwimu za idadi kubwa ya wanafunzi wanaofaulu darasa la saba na kuendelea na masomo ya sekondari, lakini tukielezwa kwamba hawajui Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.

Kwa hakika kabisa, ni jambo ambalo linaumiza kichwa kwa sababu katika mfumo rasmi wa elimu katika nchi hii, kuna mitihani ya kupima uelewa wa wanafunzi kuanzia darasa la nne, ambayo lengo lake ni kuwachuja wanafunzi wanaopaswa kuendelea na masomo ya darasa la tano, kabla ya kuufikia mtihani wa Taifa wa darasa la saba.

Kutokana na mfumo huo, maana yake ni kwamba wanafunzi wote waliopita darasa la nne na hatimaye kufika darasa la saba, wana uwezo kitaaluma. Kwa hiyo, zinapokuwepo taarifa za wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, ambao hawawezi hata kuandika majina yao, hilo kwa kiasi fulani linakuwa ni jambo la kushangaza.

Agosti 14, 2013, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, akizungumza kwenye Warsha ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa, iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya watendaji wa elimu ngazi ya kanda, mkoa na wilaya, naye alikiri kushangazwa sana na taarifa za kuwepo na wanafunzi wanaofika hadi darasa la saba wakati hawajui kusoma wala kuandika.

“Halafu Ofisa Elimu unawateua wanafunzi wa aina hiyo kwenda Sekondari. Tatizo liko wapi? Uteuzi wenu unazingatia vigezo vipi? Je, hakuna namna ya kuthibitisha wale waliochaguliwa wanajua kusoma na kuandika? Maofisa Elimu mnashirikiana vipi na walimu wakuu katika hili?”alihoji Dk Kawambwa katika warsha hiyo.

Kwa sasa, Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi kila mwaka bila kuwa na stadi za kujua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK), huku baadhi yao hao wakifikia hata kuchaguliwa kuanza kidato cha kwanza.

Takwimu kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) zilizokusanywa katika mikoa yote ya Tanzania Bara katika miaka ya hivi karibuni, ambazo FikraPevu inazo, zinaonyesha kwamba wastani wa chini kabisa wa idadi ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba bila kuwa na stadi za KKK katika kila mkoa ni 200, huku wastani wa juu ukiwa ni wanafunzi 400.

Aidha, akijibu maswali ya wabunge bungeni mwaka huo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo alisema katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2010, asilimia 88 ya wanafunzi wote waliomaliza mwaka huo, walipata daraja la nne na sifuri, huku asilimia 12 tu wakipata daraja la kwanza hadi la tatu, huku akibainisha pia kwamba asilimia 31 ya Watanzania wote nchini walikuwa hawajui kusoma na kuandika.



Wanafunzi wa darasa la awali wapatao 90 katika shule ya msingi Puulu wilayani Nyasa mkoani Ruvuma hali inachangia kukosa stadi za KKK

Takwimu zote hizo TET na Wizara, ni ushahidi tosha kwamba kuna jitihada za ziada zinazotakiwa kuikomboa nchi hii kutoka kwenye dimbwi la ujinga. Ongezeko la wanafunzi wanaopata daraja sifuri, linakwenda sambamba na ongezeko la watu wasiojua kusoma na kuandika.

Ikumbukwe kuwa katika miaka ya 1970 na 1980, Tanzania iling’ara katika nchi za Bara la Afrika, hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara, kutokana na kasi ya kupunguza idadi ya wananchi wake wasiojua kusoma na kuandika.

Chini ya Sera ya Elimu ya Watu Wazima, nchi iliongeza idadi ya watu wanaojua kusoma na kuandika kila mwaka. Manufaa yake yalionekana bayana kwa kuwa watu waliweza kupambana na changamoto zinazowakabili, ikiwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao mashambani kutokana na kuzingatia elimu ya kilimo bora, sambamba na kuongeza uelewa wa kujikinga na maradhi mbalimbali.

Hadi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere anang’atuka madarakani mwaka 1985, idadi ya Watanzania waliokuwa hawajui kusoma na kuandika ilikuwa ni takriban asilimia tisa (9) tu. Kwa hiyo, kama Taifa, kama tungefanikiwa kuendeleza kasi hiyo ya wakati wa Mwalimu hadi mwaka 2010, tungekuwa na angalau asilimia 95 ya Watanzania wanaojua kusoma na kuandika, sawa na asilimia tano (5) ya wasiojua kusoma na kuondika.

Kuongezeka kwa idadi ya wananchi wasiojua kusoma na kuandika kutoka asilimi tisa mwaka 1985 hadi asilimia 31 mwaka 2010, ni ushahidi tosha kwamba Taifa hili linarudi nyuma kwenye ujinga badala ya kusonga mbele. Historia ya Elimu ya Watu Wazima inaonyesha kwamba ilipofika Agosti mwaka 1975, Tanzania ilikuwa ni nchi ya kwanza ulimwenguni kufanya mtihani wa kisomo kwa watu wazima wapatao zaidi ya milioni 3.8, sawa na asilimia 77 ya watu wazima wote waliokuwa wanahudhuria madarasa ya kisomo hicho.

Aidha, mwaka 1981, Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza katika nchi za ulimwengu wa tatu, kuanzisha kampeni ya kitaifa ya kisomo cha kujiendeleza iliyohusisha watu wazima zaidi ya milioni 1.4 waliofuzu kisomo katika hatua ya nne. Ingawa hivi sasa juhudi zimeanza upya, huku mipango thabiti ikiwa imeandaliwa kwa lengo la kufufua upya kisomo cha kujiendeleza, uchunguzi uliofanywa na FikraPevu umebaini kuwa Taifa hili linakabiliwa na tatizo kubwa la ujinga wa kutojua kusoma na kuandika kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Tanzania.

Kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2002, pamoja na matokeo ya tafiti mbalimbali zilizopo, ilikadiriwa kwamba idadi ya watu wazima waliokuwepo katika nchi hii, ambao walikuwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu, walikuwa ni milioni 5.5, sawa na asilimia 32 ya Watanzania wote wa mwaka huo. Miaka 10 baadaye, kwa maana ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, idadi ya watu ambao hawakuwa wakijua kusoma, kuandika na kuhesabu, ilifikia jumla ya watu takriban milioni 11, sawa na ongezeko la ujinga mara mbili ya ule wa mwaka 2002.

Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa katika Sekta ya Elimu, ambao umeamua kuwaondolea mrundikano wa masomo wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili, na kuwabakiazia masomo matatu tu ya Kuandika, Kusoma na Kuhesabu, pengine ni mikakati unaoweza kusaidia kupunguza tatizo hili la wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza bila kuwa na stadi yoyote ya KKK.

Hii ni changamoto mpya kwa Serikali, kupitia Wizara ya Elimu katika kuhakikisha kwamba mtaala huo mpya wa kujenga stadi za KKK katika shule za msingi, unatekelezeka kwa vitendo ili kuinusuru nchi hii kutoka katika wimbi kubwa la watu wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu.
 
Elimu ya watanzania!!!!
Labda uliyoyasema ni kweli, lakini haohao unaowaita vilaza ndio;
Wanunuzi wakubwa wa bidhaa zenu za viwandani,
Wanawauzia na nafaka za kula na kufanyia biashara, wanawaajiri ktk shule na mahoteli yao.
Nimegundua mnachuki, hila na kijicho sana na tanzania, mnatamani hata majanga yatupate.
Huishi kuutafuta ubaya wa watanzania kwanini?
Kama tz ni kikwazo kwanini msiendelee na nchi zingine?
Tz bila kenya tutaishi bila shida.
Ninajua mnaihitaji sana tz kuliko tz kuihitaji kenya.
 
Kwani mmelazimishwa kuungana na watu wenye elimu duni???je nyinyi hiyo elimu hadi sasa imewasaidia nini mbona mnakufa,njaa,ugaidi,kutokua na ajira au hizo shule zenu mnasomea wizi,uwongo,roho mbaya na majungu???
 

Nchi zetu zinahitajiana kwa njia moja au nyingine, lakini ndio pawe na uwiano wenye manufaa baina yetu, ni bora elimu ingekua mfumo wa kutuunganisha. Lakini kwa tulivyo sasa, itakua kila siku mnasuasua kwa kila hatua, kumbe tatizo ni elimu.
Tutakua tunawalaumu kwa mwendo wenu wa kobe bila kujua tatizo lipo hapo kwenye vitabu.

Nashauri tuunganishwe kielimu, tuwe na mtaala mmoja, mfumo mmoja wa elimu.
 
Tatizo la hao wakenya ni kulazimisha kutumia fursa za watanzania ilihali hao watz wapo viongozi wa sasa tz tofauti na hao wazamani ndio mliwapeleka puta huo muungano sio wa muhimu kama maslahi ya watz hayatakuwepo

Kiongozi, taarifa inaongea kuhusu matokeo ya elimu yenu kwa miaka ya hivi majuzi. Hata mwaka jana... Sasa hao ndio Watanzania mnaojiita wa leo jameni kwenye mfumo duni kiasi hicho. Bora hao wazee wa hapo awali, kidogo walizingatia elimu, sidhani kama waliachia mwanafunzi anafikia kufanya mtihani wa mwisho kama hajui kusoma wala kuandika.

Hatari, maana inawafanya mnawaogopa Wakenya linapokuja suala la kufanya chochote kwa pamoja. Hadi mnasuasua kwa kila hatua.
 
Jirani mapenzi niliyonayo kwa jirani zangu ninaonyesha hali halisi ya maisha ya jirani.

Asante, nayahisi hayo mapenzi yako, tatizo kwa kutupenda sana unajikuta unachanganyikiwa na kupika recipe isiyo, kule jikoni.
 
Ninawapenda sana jirani lakini msinichinje ninaomba maana kuona damu kwenu ni kawaida.
 

Safi, japo hapa tunaongea kuhusu uwezo wa watoto kusoma na kuandika. Mada sio kuhusu miundo mbinu ya shule, kuna wanafunzi wanaosomea vijijini kwenye hali ngumu lakini wanapita mitihani hata kuwaliko wale wa mjini. Na ndio maana tuliamua kuwapa laptops hata huko huko kijijini, cha msingi ni uwezo wa mwanafunzi.
 
Ninawapenda sana jirani lakini msinichinje ninaomba maana kuona damu kwenu ni kawaida.

Hehehe!! Wala usiwe na wasiwasi kutuhusu, waulize wanawake wa kutokea Rombo wanatupenda sana. Hapa Nairobi mademu tumeoa wengi kutokea Bongo. Kwanza kuna jamaa hapa kavua toto toka Iringa, mwanamke wa Kimbena. Huwa haoni hiyo damu....
 
Hahahaha, mbona mnalilia sana huo muungano?
Where is CoW?
Why don't you just proceed with it,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…