Huyu jamaa nilisoma naye Mara sec school alikuwa rafiki yangu wa karibu sana ingawa baada ya kumaliza o level yeye alienda shule nyingine na mimi kwenda shule nyingine lakini tuliendelea kuwasiliana na kuwa karibu. O level halikuwa hana uwezo kabisa alichukua masomo ya Art. Lakini alikuwa mwizi mkubwa sana wa mitihani mpaka alituletea matatizo makubwa sana kipindi hicho kwa ajili ya wizi( waliosoma mara sec school 1992-1995 watakumbuka), baada ya hapo alienda Mkwawa aliendeleza ishu yake ya wizi wa mitihani, UDSM nasikia aliendeleza ishu ya kuiba mitihani. UDSM alikuwa anasoma kiswahili.