1. Shule ya msingi, John Mnyika alikuwa mwanafunzi wa kwanza kwa mkoa wa darisalama. Akachaguliwa kwenda Ilboru lakini akaamua kwenda seminari. (Naachana na hili kwa kuwa ni swala la kiimani)
2. Form 4 akapata A masomo tisa. Katika mwaka ambao matokeo yalikuwa na mushkeli kwa uvujaji wa mitihani. Angeweza kwenda shule yoyote na mchepuo wowote. Akaamua kwenda Tambaza.
3. Form 6 akapata matokeo mazuri tuu (ambayo hayakuwekwa wazi kama matokeo ya form 4)
4. University akaamua kusoma evening classes. (Hakumaliza kwa sababu alizozitaja hapo juu)
Kwa wenye busara, mlolongo wa elimu wa huyu bwana unanuka samaki aliyechina. Mimi binafsi nimesoma Tanga school, wakati wa headmaster Tetti. Wakati sisi tuko O'level pale Tanga school alikuja mwarabu mmoja kujiunga form 5 (PCM) tulikuwa tunamwita "yarabi salama". Yarabi salama yeye wakati akiwa form 5 PCM alikuwa haelewi kwa nini namba ikitoka upande mmoja wa equation na kuvuka alama ya sawasawa na kuhamia upande mwingine mwingine, basi inabidi alama yake ibadilike, kama hasi itakuwa chanya na chanya huwa hasi. Form 5 PCM huyo. Na bwana yarabi salama alikuwa amepata alama A katika hesabu O level. Baadaye ikagundulika kwamba wakati wenzake wanafanya mitihani, yeye alikuwa anazaa mitihani.
Sijui kama msamiati wa kuzaa bado unatumika siku hizi, lakini kuzaa maana yake ni kwamba kuna watu wana networks na mitihani inapotoka na wanapoingia kwenye chumba cha mtihani, hawaji kufanya mtihani ispokuwa wanakuja na "booklet" zao ambazo maswali yanakuwa tayari yameshafanywa. Sasa wakati wenzao wanafanya mtihani wao wanaandika namba yao ya mtihani tuu kisha wanazaa.
a) Sasa, najiuliza. Mnyika amesema kwamba alikuwa wa kwanza mkoa wa darisalama. (Sibishi, lakina Sijui amejuaje)
b) amepata A tisa form IV; lakini hakusema amepata A ngapi form VI. Jee inawezekana ni kwa sababu matokeo yake ya form 6 hayashabihiani na yale ya form 4?
c) A tisa, lakini hakwenda Ilboru. Kwanini mwanafunzi hodari asiwe na hamu na shauku ya kusoma na wanafunzi hodari wengine? Jee inawezekana bwana Mnyika alikuwa anaogopa "to get found out?"
d) Baada ya kupata matokeo mazuri form 6; kwanini asome jioni? Jee alikuwa anaogopa kusoma na wanafunzi hodari?
e) Mpaka leo bado hana degree. [anisamehe kama nimekosea katika hili]. Ni kweli mwanafunzi mwenye uwezo wake wa kitaaluma atakubali kuishia njiani kwa namna aliyoishia yeye?
Sasa kila nikimtafiti huyu bwana Mnyika, samahani, lakini neno kuzaa linapiga kengere zote akilini mwangu. Nadhani huyu bwana ni miongoni mwa wale wenye bahati nzuri ambao huweza kuipata mitihani kabla ya siku ya mtihani.