Kumeibuka na sintofahamu juu ya elimu ya wabunge, wa darasa la saba wanawaponda maprofesa, maprofesa wanajimwambafy. Wananchi wanatoa maoni juu ya umuhimu wa elimu kupambanua mambo.
Sasa kama ndio hivyo mtu aliyepata div 0 anatofauti gani na aliyeishia la saba, je ataweza kupambanua mambo? Nape inasemekana alizungusha form four. Sasa Iq yake kupambanua mambo imekaa vipi?
Hii ndio hadithi iliyopelekea kurejea matokeo ya div "0" ?
Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema kwa mujibu wa nyaraka za chama hicho tawala, kukosoa na kujikosoa ni silaha ya mapinduzi na kujiimarisha na si dalili ya udhaifu.
Nape ameyasema hayo leo Alhamisi Aprili 15, 2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu na taasisi zake kwa mwaka 2021/22.
Amesema Rais wa awamu ya sita, Samia Suluhu Hassan ameanza vizuri na kutaka wananchi kumpa ushirikiano, “mzee Mwinyi (Ali Hassan- rais wa awamu ya pili) alituambia kila zama na kitabu chake.”
Amebainisha kuwa wamekuwa na vitabu vitano akirejea marais watano Julius Nyerere, Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli akisisitiza kuwa wito wake kwa viongozi, wabunge wenzake, wanachama wa CCM pamoja na Watanzania kumsaidia Samia kwa kumuunga mkono aandike kitabu cha awamu ya sita.
“Mhe. Naibu Spika kwenye Document zetu, tumesema kujikosoa na kukosoana ni silaha ya mapinduzi na kujiimarisha na sio dalili ya udhaifu. Tusigombane bila sababu Tanzania ni yetu sote tumsaidie mama naye aandike kitabu chake tusimshike mkono kumwandikia kitabu tumwache aandike kitabu chake.
“Hasa ile inayofanywa na mtu kama Magufuli itajitetea na kujisimamia miaka labda kama mtu ana mashaka na legacy yake lakini kama hamna mashaka na legacy yake itasikilizwa, itaongewa sisi watoto wajukuu na vitukuu kwa sababu haya waliyoyafanya watayakuta.
“Ndugu zangu legacy (alama) haitetewi legacy inajitetea yenyewe hasa ile inayofanywa na mtu kama Magufuli, legacy yake itajitetea, itajisimamia kwa miaka, unless mtu ana mashaka na legacy yake. Legacy yake itasikilizwa, itasemwa na sisi, watoto, wajukuu na vitukuu kwa sababu haya aliyoyafanya watayakuta tu.,” amesema.
Amesema sasa hivi hawana sababu ya kugombana na hawana sababu ya kutoana macho. “Mimi nimekuwa kiongozi katika chama, nimesimamia idara ya maktaba na nyaraka duniani hakuna chama bora kilicho document vya kutosha CCM ni karibia namba moja kwa kila kitu,” amesema.
Amesema kwenye nyaraka zao wamesema kukosoa na kujikosoa ni silaha ya mapinduzi na kujiimarisha na sio dalili ya udhaifu
Sasa hiyo hadithi ya Nyepa inatakiwa iende na hadithi ya
Gwajiboy
Mbunge wa Jimbo la Kawe Josephat Gwajima akitoa mchango kuhusu hotuba iliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema nchi nyingi za Kiafrika zimekuwa haziendelea kwa kasi ya maendeleo kutokana na kushindwa kutumia rasimali kwani inaendana na 'manpower'.
Pia ameeleza kuwa Tanzania inashindwa kuendelea mbele kwa kasi kwasababu hakuna muendelezo wa Regime moja kwenda nyingine ambapo kila Rais anaingia madarakani na mipango yake hivyo huathiri maendeleo ya ukuaji wa mipango iliyoanzishwa.
Gwajima amtolea mfano Nyerere alietawala miaka 20 na kuacha viwanda 411, alipokuja Mwinyi aliboresha baadhi ya mambo lakini hakuendelea na wazo la viwanda na alipoingia Mkapa akauza vyote kwa kuvibinafsisha hivyo kukosa muunganiko kati ya 'regime' ya kwanza na regime ya tatu.
Gwajima amesema watakesha kama hamna huo muunganiko kwani hata Rais wa awamu ya nne hakushughulika na viwanda, bali mambo mengine lakini awamu ya tano akaamua kushughulika na viwanda, vilevile ambavyo awamu ya tatu ilivibinafsisha na kuviuza.
Gwajima amesema ni hatari kwasababu katiba inampa nafasi kila Rais anayeingia madarakani kwa namna yake, hekima yake na kwa namna anavyotafasiri yeye maendeleo.
Amesema siku moja atakapopatikana Rais ambaye hayuko sawasawa watu wataishia kulia na kutoa ombi la kuwa na vision ya kuwa na miaka 50 ya Taifa na anapoingia Rais lazima ilani ya chama chake izungumze mambo ambayo Taifa imejiwekea kama maono.
Gwajima amehoji endapo akatokea Rais ambae anafanya mambo yake yasiyo kwenye ilani kama kuna mtu wa kumuuliza mwenyekiti wa chama cha mapinduzi na Amiri Jeshi mkuu!
hivyo legacy ya kiongozi yeyote itakuwa ktk usimamimizi wa sera na muelekeo wa kiuchumi
We nchi iwe kwa pole au ikali na sio kuharibu sifa ya mwingine hususan akiwa "amefariki" hawezi kutetea