Elimu ya Tanzania haichangii chochote kwenye global science and technology kwasababu inahabiribiwa na mwingiliano wa lugha baada ya miaka 7 kuanzia kidato cha kwanza.
Hapo juu ni mada:
Karibuni tujadili kiundani:
Mimi nitatoa highlights zangu chache hapa:
Kuanzia kidato cha kwanza wanafunzi wanabadirishiwa mfumo wa lugha ya kujifunzia kutoka kiswahili na kuanza kutumia kiingereza.
Wanaanza darasa la nane (8) (kidato cha kwanza) kama darasa la kwanza, wanaanza kupambana na lugha na kushika vitu wasivyo vielewa ili kuokoa muda. Wanaweza kutumia hata miaka minne yote wanashika tu vitu hawaelewi kiundani.
Walimu wanaita kushika point,
Mwanafunzi wa Marekani, China, Kenya, Urusi, Uganda, yeye anapofika darasa la nane hahitaji kukariri vitu asivyovielewa kwasababu tayali yeye alishaizoea lugha kila kitu anakwendwa kwa kuelewa. Hii ndio faida ya kutumia lugha moja kuanzia darasa la kwanza.
Hapo ilitakiwa waendelee na lugha ile ile waliyoizoea kuanzia darasa la kwanza.
Naweza kusema hapo kuanzia kidato cha kwanza ndipo uharibifu wa elimu yetu unapoanzia. Mtu hawezi kufanya vumbuzi kama wanazofanya wenzetu kwa kuwa na mfumo kama huo unaochanganya lugha mbili kwenye elimu. Inatakiwa tuwe systematic tuchague lugha moja ya kufundishia ndipo tutaweza kushindana na mataifa mengine katika elimu.
Reference.
1 . Introduction Any country that intends to stand out among other nations of the world and to be able to assert without being afraid that they are enlightened should be capable of pointing out also that they are well-developed nation .
www.modernghana.com