Nunias Mathayo
New Member
- Jun 22, 2023
- 2
- 2
ELIMU NI MSINGI BORA WA MAENDELEO KATIKA NYANJA ZA KIJAMII ,KISIASA NA KIUCHUMI KUPITIA MFUMO WA ELIMU TANZANIA
ELIMU ni maarifa yanayopatikana kwa njia ya kujifunza au kusikiliza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingne ili kuwa na uelewa juu ya jambo flani linalohusu jamii,uchumi na siasa bora na maendeleo ya mtu mmoja mmoja.Elimu ya Tanzania Ina umuhimu sana kuwapatia watu fursa ya kujiajiri wenyewe na kuendeleza shughuli za kiuchumi na kisiasa pamoja na jamii kwa ujumla. Elimu ni muhimu sana katika maendeleo ya kiuchumi na kisiasa, na kuimarisha mfumo wa elimu nchini Tanzania ni jambo la kipaumbele. Ili elimu ya Tanzania iwe na umuhimu wa watu wote kwa wale ambao wamepata FURSA ya kuingia darasani au wamepitia njia mbalimbali ya kujifunzia mfano mikutano ya KIBIASHARA. Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya elimu kuna baashi ya vitu lazima ivizingatie na kuvihimarisha kwa ajiri ya kuleta mabadiliko makubwa nchini,
1. KUIMARISHA MTAALA WA ELIMU
Mtaala wa elimuu napaswaa kuwa na manufaa kwa kuandaa wanafunzi kwa ajira na shughuli za kiuchumi. Mtaala unapaswa kuzingatia ujuzi unaohitajika katika soko la ajira, kama vile ujuzi wa kiufundi, stadi za ujasiriamali, na ujuzi wa teknolojia. Pia, mtaala unapaswa kujumuisha mafunzo ya kujenga uwezo wa kisiasa na uongozi.
2. KUWEZESHA MAFUNZO YA UFUNDI NA STADI ZA UJASIRIAMALI
Programu za mafunzo ya ufundi zinaweza kuimarishwa ili kutoa ujuzi unahitajika katika sekta MBALIMBALI za kiuchumi. Vilevile, mafunzo ya stadi za ujasiriamali yanaweza kusaidia kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuanzisha biashara zao wenyewe na kuajiri wengine. Serikali inaweza kushirikiana na sekta binafsi ili kuhakikisha mafunzo haya yanapatikana kwa urahisi.
3. KUKUZA ELIMU YA UFUNDI NA TEKNOLOJI
Kuendeleza elimu ya ufundi na teknolojia kunaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuwawezesha watu kujiajiri wenyewe. Kuanzisha na kuimarisha vyuo vya ufundi na vituo vya teknolojia itatoa fursa kwa wanafunzi kupata ujuzi unaohitajika katika sekta za kisasa na kusaidia kuendeleza shughuli za kiuchumi.
4. KUWEZESHA MAZINGIRA YA KIBIASHARA
Ni muhimu kuboresha mazingira ya kibiashara ili kuwapa watu fursa ya kuanzisha na kuendesha biashara zao. Serikali inaweza kuchukua hatua za kuondoa vikwazo vya kisheria na kutoa msaada kwa wajasiriamali, kama vile mikopo yenye riba nafuu na mafunzo ya usimamizi wa biashara
5. KUHAMASISHA UTAYARI WA SIASA NA UONGOZI.
6. KUTOA FURSA (AJIRA) KAMA SEHEMU YA KUENDELEZA SHUGHULI ZA KIUCHUMI KATIKA SEKTA YA VIWANDA.
sehemu ya kuendeleza shughuli za kiuchumi hasa katika sekta ya viwanda. hii itachangia sana katika makuzi ya kiuchumi kwa sababu wapo ambao wamesoma na wamefika level ya juu na Wana ujuzi wa mkubwa na ustadi wa kuendelea kupambania maendeleo ya Tanzania mfano katika sekta ya viwanda kuna wimbi la kuleta wataalamu kutoka nje ya Tanzania (foreign experts) hii inasababisha baadhi ya wataalamu kutoka Tanzania hukosa nafasi ya KUAJIRIWA (unemployment). Na tena mashuleni wanafunzi wapewe motisha ya kusoma mosomo ya SAYANSI ambayo ni njia mojawapo ya kuwapa wanafunzi uelewa na ustadi mkubwa juu ya teknolojia.
Upvote
3