Ricky Blair
JF-Expert Member
- Mar 13, 2023
- 562
- 1,148
Tanzania sio kisiwa na pamoja na sio kisiwa bado ni nchi masikini duniani na ivyo Kiswahili chetu bado hakitatupaisha sana duniani sio kama Kichina, Kijapani au lugha zingine duniani kwenye nchi tajiri.
Cha Kwanza; Kiswahili ifundishwe kote kutoka primary hadi chuo kikuu kama lugha kuu ila Kiingereza kibaki kufundishwa tangia chekechea kama somo pekee na watoto wafundishwe vizuri sio hii medium of instructions kiswahili kisha unahamia kiingereza ukiingia secondary, haileti maana na ndo maana watanzania wengi hata walioenda shule hadi chuo bado kiingereza wako very poor. Ivyo turekebishe ivo bila kuondoa kiswahili as medium of instructions kwani Israel, Netherlands, Norway, Sweden, Finland, Denmark hadi Portugal bado wanatumia lugha zao kw sekta zote ila Kiingereza wanaongea vizuri 90% na wako fluent wakati TZ hata 10% ukiwapata ni kwa shida.
Kiingereza ni lugha ya dunia tayari kwaiyo sina haja ya kusema umuhimu wake sana kwa sababu ina waongeaji asili zaidi ya milioni 400( USA, UK, Australia, Canada, New Zealand, Ireland etc) na inazingumzwa na mamilioni uko Asia kama India na Africa kama Nigeria, South Africa na former British colonies. Ni lugha kuu ya biashara, sayansi na utafiti wote wa sayansi na kwenye internet zaidi ya 50% zipo kw kiingereza. So kiingereza hakina mshindani.
Pia watoto wakiwa primary; wapewe option ambao wazazi wao wanaweza kuwachagulia wasome lugha nyingine kati ya hizi;
Kifaransa
Kireno
Kihispania
Kijerumani
Kiarabu
Kichina
Na lugha nyingine yoyote ya Africa ambayo ina waongeaji wengi kama Hausa, Zulu, Amharic etc
Kifaransa ni muhimu duniani ukiachana na Nchi ya France yenyewe tu, former colonies zote kama DRC, Congo ya Brazaville, Senegal, Ivory coast, Rwanda, Burundi etc ina mamia ya milioni ya waongeaji na ndo maana pia ni lugha ya African union.
Kireno pia ni muhimu ukiachana na Ureno yenyewe ambayo ina watu milioni 10 tu, Brazil ina mil 200 na Angola na Mozambique zaidi ya mil 35 na zinazidi kukua na makoloni mengine.
Kihispania pia tukiachana na Spain na Equatorial Guinea ambayo ndo nchi pekee ya Africa wanayoongea; Latin America yote kuanzania Mexico hadi Argentina ( Chile, Bolivia, Colombia, Venezuela, Cuba, Honduras, Guatemala, El Salvador, Nicaragua, Paraguay, Uruguay etc) wanaongea Spanish na watu zaidi ya milioni 500 na ni lugha ya pili Marekani inayozungumzwa sana.
Kiarabu pia ni lugha kuu Africa na Uarabuni na ina waongeaji zaidi ya mil 300 pia so ukiijua hii itafungua milango mingi ya nafasi uko mbele kama lugha zingine
Kijerumani; ingawa legacy yao ya kikoloni kama Italia imekufa Africa; bado Kijerumani ni muhimu kwani ni nchi yenye uchumi mkubwa Ulaya na baba mkuu wa EU. Ina watu zaidi ya 85m na ni mtengenezaji mkuu wa vitu vingi duniani na uchumi wa 3 duniani sasa ivi akiwa ashampita Japan. Pia Austria na Switzerland wanaongea kijerumani.
Kichina; ina watu 1.4 billion na nchi ambayo ina uchumi mkubwa duniani wa pili baada ya Marekani na very soon itaipita Marekani. Kufanya biashara na China sasa ivi haiepukiki na kuna faida nyingi sana ivyo kujifunza lugha yao.
Kama nilivyosema awali. Kiswahili kifundishiwe kama lugha kuu na kiingereza somo tofauti ila akiwa primary achaguliwe lugha kati ya nilizozitaja za kujifunza kama somo lingine ila asizidishwe zaidi ya 2. Mfano anaweza chagua Spanish na Kireno au Kijerumani na Kichina au Kichina tu au kiarabu tu.
Akiingia secondary atachagua tena moja au mbili kama ataweza kumudu na akiingia chuo anaweza kuchagua zingine.
Kuna umuhimu sana kujua izi lugha kwenye dunia ya sasa ya upanawazi na ajira za mtandaoni na kuna kampuni nyingi za Ulaya au popote wanaweza kukuajiri kama customer care ukiweza kujua lugha zao na unaweza kufanya kaz online. So usidharau wadau hata kuwalipia watoto zenu binafsi waanze kujifunza ili akiwa na miaka 24( ukiachana na lugha yake mama Kiswahili au na lugha zingine za kikabila, anajua English fluently pia anaongea labda Kireno, Kihispania na Kichina au anajua Kifaransa, Kijerumani na Kiarabu) Niamini CV yako itakuwa nzito kuliko mtu anayejua kinyakyusa, kiswahili na kiingereza cha kubahatisha. I rest my case.