Elimu ya Tanzania imegubikwa na ubabaishaji mwingi hasa inapofikia wakati wa kutangaza matokeo, hadi leo hii tar4 matokeo ya kidato cha sita hayajatangazwa na hakuna ajue yatatangazwa lini licha ya tetesi za hapa na pale zinazotolewa na wale wanaojiita wadau wa elimu. Swali ninalojiuliza ni kwanini utangazaji matokeo umekuwa ukichelewa? Na matokeo yanapotangazwa jamii ushuhudia matokeo mabovu?