Elimu ya Tanzania sio elimu ya kujiajili mbali ya kuajiliwa

Elimu ya Tanzania sio elimu ya kujiajili mbali ya kuajiliwa

Matandu

New Member
Joined
Mar 6, 2013
Posts
3
Reaction score
1
Kwa mtazamo wangu,elimu ya Tanzania sio elimu ya kujiajili mbali kuajiliwa hivyo basi hatuwezi kushindana na nchi mbali mbali katika nyanja ya maendeleo hususani katika sayansi na tekinolojia.Vijana wengi wakisha hitimu vyuo hushindwa kujiajili kwa sababu elimu waliyopata haiendani na matarajio yao,yaani haiwapi ujuzi wa kupambanua mambo namna ya kukabiliana na maisha.Mfano mwanafunzi kuanzia shule ya msingi anasoma ukoloni mpaka chuo na anahitimu hivyo hivyo,mhitimu wa namna hii ataonesha mabadiliko yoyote kwa jamii? Nathubutu kusema mara zote ukiwapambanisha kimaisha na aliyesoma na ambaye hajasoma,ambaye hajasoma maisha yake huonekana ni bora na ni mjuzi zaidi ya aliyesoma,katika elimu ya kitanzania matini tunazotumia hutoka Marekani,Uingereza etc.hayana kabisa uhusiano na mazingira yetu hivyo inatupasa kusoma hayo matini kwa kukariri.Mbona tunawasomi wengi,kwa nini wasifanye mapinduzi katika sekita ya elimu? au kwa kuwa wamepitia katika mfumo huo huo wanashindwa kuleta mabadiliko? Mimi sikubaliani kabisa na mfumo wa elimu nchini tunahitaji mabadiliko,pia siasa imekuwa mnara wa kuongoza elimu,mitaala inabadilika mara kwa mara kwa sababu ya wanasiasa.Ukitazama nchi zote zilizoendelea,elimu yao iliendana na mazingira yao.ELIMU KWANZA MENGINE BAADAYE
 
Huo ni mtazamo wako. Lakini nakushauri ukifikiri usawa wa pua utaishia kulalamika miaka yote. Mbona wengine tumesoma na tumejiajiri na kuajiri wengine kwenye miradi yetu na turnover zetu kwa mwaka ni kubwa tu. Think outside the box. Chukua hatua hacha kulalamika.
 
Back
Top Bottom