Elimu ya vyuo vikuu Mwanza

Joined
Jan 19, 2017
Posts
14
Reaction score
28
Jiji la Mwanza, la pili kwa ukubwa Tanzania (The second largest City in Tanzania), sifa nyingine ni jiji lililo katikati Kati ya majiji ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, hapa namaanisha Nairobi, Kampala, Kigali, Bujumbura. Kinshasa pote ni karibu kufika jijini Mwanza.

ELIMU YA JUU

Katika elimu ya juu hapa jiji la Mwanza limechelewa sana, yaani hakuna chuo hata kimoja kikuu cha serikali , kitu ambacho kinakichekewesha sana jiji la Mwanza kimaendeleo Kama jiji na kusomeka vizuri katika ulimwengu duniani Kama kitivo cha elimu.

Ikumbukwe jiji la Mwanza lina vyuo vikuu viwili vya binafsi vinavyomilikiwa na taasisi ya dini , amabvyo ni CUHAS ( Catholic University of Health and Allied Science) pia SAINT AUGUSTINE UNIVERSITY OF TANZANIA au maarufu Kama SAUT .

Ukiachana na vyuo hivyo Kuna taasisi tu tena ni kampasi za vyuo vya sehemu nyingine, hapa namaanisha Taasisi ya mipango vijijini (IRDP) -Mwanza, Tassisi ya uhasibu Tanzania ( TIA), College of Business Education ( CBE) - Kampasi ya Mwanza, chuo cha usimamizi wa fedha (IFM)- Mwanza Kampasi , chuo kikuu huria ( OUT) - Mwanza , Taasisi ya teknolojia Dar es salaam ( DIT) -Mwanza.

Hivyo vyuo vyote havijakidhi mahitaji ya watu wa ukanda wa ziwa na magharibi ambapo kuitafuta elimu inabidi wasafiri umbali mrefu sana, mikoa hiyo ni Mwanza , Shinyanga, Simiyu, Geita, Kagera, Mara, Tabora , Kigoma , Katavi , Rukwa n.k

Kiuhalisia wengi wanaotoka Kanda ya ziwa husoma fani za uhandisi, madini, sheria na biashara pia udaktari , katika kundi kubwa , kuipata elimu hiyo katika vyuo vikuu Hadi waende umbali mrefu sana.

Sijawahi kuona mpango mkakati wa chuo kikuu jijini Mwanza zaidi ya Kampasi tena za taasisi tu na sio vyuo vikuu.

Hapa serikali ilijisahau sana au pengine Mwanza haikupata wabunge wenye ushawishi bungeni juu ya suala la elimu , hivyo kuachwa nyuma sana.

Kama mdau wa elimu Kuna haja serikali kuweka mradi mwingine was chuo kukuu , hiki kijengwe jijini Mwanza either maeneo ya Kisesa au Wilaya ya Misungwi , kiwe Kama chuo kikuu cha Dodoma kibobee zaidi katika uhandisi , madini , biashara na masuala ya teknolojia namaanisha IT, Telecom, Computer Science na Engineering na mambo mengine mengi mazuri.

Na Kama uwezo wangu chuo hicho kiitwe University of Mwanza (UoM) . Kiendane na kasi ya mabadiliko ya ongezeko la watu, na watu wengi ukanda wa ziwa wapate elimu pia kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kati.

Viongozi wa serikali pitieni uzi huu. Naamini nimetoa mawazo yangu.
Nawasilisha wenu Malika.
 
Vyuo vikuu kama UDSM havikuwekwa kwasababu huko kuna yale makabila makubwa tu.

vikabila vidogo vingeteseka sana endapo makabila makubwa yangeanza kupata elimu.

Maana wengi wangesoma sana na nchi ingekuwa kikabila zaidi kama Kenya. Hivyobasi ili kubalance, ikabidi vyuo vikuu vijengwe huku changanyikeni ili kusudi mpaka wasomi wakishakuwa wengi changanyikeni, hata huko mwanza ama bukoba vitajengwa na ukabila utakuwa haupo tena, ratio itakuwa imebalance na watu wote watakuwa wameelimika kwa kiwango sawa. Na nchi itaenda vizuri. Nyerere alikuwa anaona mbali sana.

Nadhani nimekujibu.
 
Nafikiri hujasoma uzi vizuri , umeenda kwenye ukabila badala ya kujua malengo ya uzi huu Ni kujengwa chuo kingine kikuu ukanda wa ziwa
 
Katika moja jambo alilotakiwa jembe kufanya kanda ya ziwa si uwanja wa chato ,wal lile dalaja alitakiwa kujenga chuo moja matata sana kanda hii hapo ningempa 5 kubwa
 
Mkuu mimi naweza kuchangia kwa kusema kwamba wasukuma na maswala ya Elimu wameanza juzijuzi nipo huku kanda ya ziwa nimejiridhisha hawa jamaa civilization bado sana na hawawezi kukomalia hilo unalolisemea hapa wao labda wajengewe chuo cha mambo ya jadi itakua poa sana ila sio elimu ya juu
 
Unatokea wapi ambapo wote mmesoma sana
 
 
Hakuna ulichoandika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…