Elimu yako ni kwa ajili ya kufaidika wewe na si jamii

Elimu yako ni kwa ajili ya kufaidika wewe na si jamii

Regent

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2020
Posts
2,306
Reaction score
3,576
Elimu uliyonayo sio kwa ajili ya kusaidia jamii, asije akakwambia mtu 'umemaliza elimu yako sasa itumie kusaidia jamii' mambo hayaendi kwa namna hii.

In capitalist era, kitu chochote utachofanya hakikisha kinakufaidisha wewe mara zote angalia mazingira yatakufaidisha vipi wewe na si mwengine au jamii...Elimu uliyoitolea jasho ni kwaajili ya kukufaidisha wewe na si mwengine hakikisha wewe unakuwa mnufaika wa kwanza na si jamii.

Jamii kufaidika na elimu yako ni baada ya wewe kuona nikifanya hiki kwa jamii nitafaidika na 123 mfano wewe ni Doctor fungua Hospital upate pesa kupitia hospital yako kuhudumia jamii...jamii inafaidika na elimu yako baada ya wewe kuona kuna faida kwa upande wako ukifungua hospital.

Usije ukamaliza chuo mtu akakwambia tumia elimu yako kusaidia jamii (Wrong), tumia elimu yako kujisaidia wewe mwenyewe hujasoma kwasababu uje kusaidia jamii.

Mambo kama kujitolea, jitolee pale tu utapoona kuna uwezekano wa kuajiriwa au kufaidika kivyovyote kwa upande wako, usije jitolea eti “nimeona nisikae bure nimejitolea nisaidie madogo” (Wrong).

Capitalist Thought zina sound kama vibaya, roho mbaya ila utapigika na Dunia ukienda against nazo (Your Life Is First Priority).

In capitalist World hata upigike vipi hakuna atakayekuja kukusaidia hapo nyumbani jukumu la maisha yako ni lako mwenyewe 100%, kwanini jukumu la kujiinua liwe lako mwenyewe si la jamii alafu wewe uwone unawajibu wa kusaidia jamii...jamii inapenda kusaidiwa yeye tu ila wewe haikusaidii.

NB:
1) Jamii ifaidike pale tu utapoona kuna faida katika kuifaidisha jamii.
2) Jamii ifaidike na elimu yako baada ya kupata faida ya kutosha na elimu yako
 
Kwa mazingira fulani naweza kukubaliana nawewe

Mana kuna mda nikijitolea kuna karoho flani hivi huniambia
"wema wangu umeniponza sasa machungu ya Dunia Nayaonjaa"
 
Mabilionea wote na matajiri wote ni watumiao elimu yao vipaji vyao au mitaji yao kusaidia jamii mfano Azam , Billy gates nk wana bidhaa zinazosaidia jamii wanawatengenrzea na kuwauzia

Elimu kama huna jamii ya kuisaidia ni hopeless hutoboi.Jamii ndio soko la elimu yako au kipaji chako au mtaji wako
 
Natamani nitengeze billboard Kubwa..kabisa ya uliyo andika...niibandike kwenye kila makutako ya barabara nchi nzima.
 
Mabilionea wote na matajiri wote ni watumiao elimu yao vipaji vyao au mitaji yao kusaidia jamii mfano Azam , Billy gates nk wana bidhaa zinazosaidia jamii wanawatengenrzea na kuwauzia

Elimu kama huna jamii ya kuisaidia ni hopeless hutoboi.Jamii ndio soko la elimu yako au kipaji chako au mtaji wako
Inaonekana hujamuelewa mleta mada....
 
Mabilionea wote na matajiri wote ni watumiao elimu yao vipaji vyao au mitaji yao kusaidia jamii mfano Azam , Billy gates nk wana bidhaa zinazosaidia jamii wanawatengenrzea na kuwauzia

Elimu kama huna jamii ya kuisaidia ni hopeless hutoboi.Jamii ndio soko la elimu yako au kipaji chako au mtaji wako
Maisha ni Utu, ubinadamu na furaha.

Ukijikita kwenye ubinafsi uliopindukia utajikuta furaha unaitafuta kwa mbinde mnooo.

Ndio maaana kuna watu wana pesa lakini wana force recognition na kukubalika kwenye jamii.

Mo huyo hapo ni tajiri, ukimwambia utajiri wako wa kurithi hajisikii Vizuri.

Jambo la msingi jitahidi kufanya kinachokupa furaha, pesa ni matokeo tu.

Jeff Bezos ana utajiri wa $200+ billions lakini kampuni yake, Amazon ina thamani ya $1 trillion.

Maana yake anewatengenezea watu wengine utajiri wa kama $800 billions.

Fanya kazi for money only if it's for survival.
 
Technically kila utakachofanya ili upate faida basi utakuwa unaisaidia jamii kwa kujua ama kutokujua.
unatoa huduma kwa jamii then inakulipa wewe ili upate faida.
Means hauwezi ukapata faida bila kusaidia jamii.
So hivyo vitu ni ngumu kutengana sababu vinategemeana

Ila kama kuisaidia jamii
Yaani wewe utoe huduma then jamii isikupe chochote kutokana na huduma yako yaani "bure".
Basi hapo upo sahihi.

Hakuna cha bure duniani.
 
Mtu mbinafsi kama wewe tukikupeleka ikulu utaanza kujilimbikizia wewe
mwenyewe, then ndugu zako, marafiki zako, mtaa wako, kijijini chako, mkoa wako, hadi ukifika hatua ya nchi umeshapinduliwa

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
In Capitalist School mimi ni Raisi ambaye kila mtu anamuota, kila Social Class inahitaji.

Nitakuwa Raisi baada ya kuona benefits kadhaa nitazopata, ili kuhakikisha naendelea kupata benefits hizo nitahakikisha nafanya majukumu yangu kwa haki na usawa bila dhambi nitaitendea nchi yangu vizuri kama
1)nitatoa ajira
2)nitapandisha mishahara
3)nitaweka mazingira wezeshi na rafiki kwa wawekezaji na wafanya Biashara
4)Nitaweka mazingira mazuri kwenye kilimo pembejeo na soko la uhakika.
5)Nitaweka mazingira wezeshi ya mitaji kwa vijana
6)Na zaidi na Zaidi

Nitafanya yote kwa Motive ya kupewa tena kula katika mitano mingine tena na tena ili niendelee kupata benefits ninazohitaji.

Uzi unahitaji Thinking Timamu kidogo
NB:
1) Jamii ifaidike pale tu utapoona kuna faida katika kuifaidisha jamii.
2) Jamii ifaidike na elimu yako baada ya kupata faida ya kutosha na elimu yako
 
Back
Top Bottom