SoC02 Elimu yenye kuleta mabadiliko kuendana na kasi ya mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia ya Ulimwengu

SoC02 Elimu yenye kuleta mabadiliko kuendana na kasi ya mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia ya Ulimwengu

Stories of Change - 2022 Competition

Jeremaya Elias

New Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Elimu yenye Kuleta mabadiliko.

Tanzania ya sasa, inauhitaji mkubwa wa elimu yenye Kuleta mabadiliko kuendana na Kasi ya mabadiliko ya kisayansi na kiteknolojia ya kiulimwengu .

Elimu hii isiwe yenye kubaki kama alama tu kwenye vyeti vya wasomiwake,bali iwe elimu ya kimapinduzi (mabadiliko ya Moja Kwa Moja).

Sayansi ni ubongo au kiini Cha ujuzi , ujuzi ambao unashikilia sehemu nyeti ikiwemo ,afya,kilimo,viwanda,uchumi, lakini teknolojia inahusisha matumizi ya sayansi ndani yake

Mabadiliko haya yakisayansi na teknolojia ndiyo yanayoisukuma Tanzania ifanane na mataifa yaliyo endelea hasa katika nyanja hizi mbili kubwa zinazo unganisha dunia kuwa kama Kijiji kimoja

Elimu hii ambayo inahitajika, ni Ile itakayo tufanya tuweze kutumia rasilimali zetu wenyewe bila yakuwa wategemezi Kwa mataifa ya nje kwani kwa njia hii tumepoteza utajiri mwingi tukidanganywa na wawekezaji mfano dhahabu nyingi zimekuwa zikisafirishwa kusafishwa nchi za nje kwenye mitambo hapo tumeibiwa sana kwani isingewezekana hiyo mitambo kujengwa nchini?

Lakini kama wangekuwepo wataalamu wazawa wangekuwa wazalendo Kwa taifa

Nchi yetu inautajiri wa rasilimali nyingi sana,tukianza na rasilimali watu ambapo kulingana na hesabu ya
watu na makazi ya mwaka 2012 , Tanzania ilikuwa na idadi ya watu 44,929,002 kulingana na chanzo cha habari cha mtandao wa tamisemi na picha hapo juu ni kutoka IPP Media kuonyesha mkusanyiko wa watu jijini Dar es salaam

Rasilimali ardhi ; nchi yetu ina ukubwa kuwa wa hekari za mraba 945,087 Pamoja na kuwa na eneo kubwa la ardhi ,pamoja nakuwa na kaulimbiu ya “kilimo ni uti wa mgongo wa tanzania” bado tanzania haina wataalamu wa kilimo wa kutosha watakao wezesha wakulima kulima kitaalamu kuongeza kipato,wakulima wamekuwa wakilima tu kwamazoea

Tuna madini yenye utajiri mkubwa tanzanite, dhahabu,almasi,bati,ulanga namengine mengi. Misitu yenye mbao ,wanyama kwenye mbuga za wanyama Lakini haya yote yamekuwa faida tu kwa- wajanja waliotuzidi ujuzi wa kiteknolojia. Shida ni elimu tunayo ipata shule .Elimu tunayo ipata shule haitufanyi tuwe wataalamu Bali kubobea katika nadharia Kwa kiwango kikubwa kuliko kuwa na ujuzi wa vitendo .

Kwani Elimu yetu inaupungufu gani?;kuwa na Sayansi yenye nadharia kuliko vitendo ;Elimu yetu imepungua baadhi ya mambo muhimu mfano mzuri ni kwenye masomo ya sayansi yanayofundishwa shule za upili yanatumia nadharia sana kuliko vitendo. Mfano shule nyingi za kata za serikali wanafunzi wengi hufahamu vifaa vingi vinavyotumika maabara baada ya kufikia madarasa ya mitihani mwishoni mwa miaka ya kimasomo hasa kidato cha nne,hapa ndipo wanafunziwengi huweza kufahamu vifaa na matumiziyake ,pamoja nayote hayo bado uzoefu wa matumizi hayo ya vifaa huwa ni shida ambapo baadhi ya wanafunzi hukwama kuunganisha mfumo wa vifaa yaani Kwa kiingereza “a set of instrument” nawakati mwingine hukwama kabisa, hii ni kutokana na kukosa muda mwingi wa kufundisha masomo kwa vitendo.

Lakini si hivyo tu wakati mwingi hufanya majaribio yaliyo gunduliwa tayari, tena wanafunzi Hulazimika kufanya majaribio hayo chini ya usimamizi wa wataalamu wa maabara yaani “laboratory technicians”kwa lugha ya kiingereza. (kama tunasema sayansi inabidi wanafunzi wafanye majaribio ya kisayansi yenye kujenga ubunifu kwenye sekta husika zinazohusiana na uhitaji wa nchi. Mfano nchini mwetu kilimo ndiyo uti wa mgongo, Kwa sababu ni Elimu yenye utekelezaji wanafunzi wafundishwe jinsi ya kuzalisha mazao yenye kukomaa haraka,kutoa mazao mengi,kuvumilia wadudu kupitia hiyo sayansi ,nasiyo kutumia nadharia zisizo na mchango wa Moja Kwa Moja Kwa jamii ya kitanzania

Uchache wa mafunzo ya muda mfupi yanayoweza kuwajengea wanajamii uwezo wa kuvuna utajiri wa rasilimali zao. Serikali yetu inatakiwa iongeze nguvu katika mafunzo ya muda mfupi ,jamii Ina uhitaji mkubwa sana wa baadhi ya mafunzo na vitendeakazi ili iweze kufaidi utajiri wa nchi yao,mfano watuwengi husikia tu almasi,dhahabu,tanzanite,bati. Lakini wengi hawajui madini haya yakoje,wengi hawajui thamani ya madini hayo,Wala kivipi yanaweza kuchochea uchumi na ustawi wa taifa lao.

Kitu cha kipekee serikali Inachotakiwa kukifanya ni kutoa mafunzo Kwa wanajamii wake,kufundisha njia sahihi za uchimbaji madini zenye kulinda uhifadhi wa baadae yaani” sustainable mining resources” pamoja na kuwa muelekezaji wa masoko au kuwa mnunuzi wa Moja Kwa Moja .Elimu isiwe ile inayotolewa darasani pekee kwani baadhi ya wasomi wanaohitimu kutoka kwenye

Huo mfumo wanakuwa hawana cha kuisaidia jamii,kwani wengi hujengewa mfumo wa nadharia zaidi Bali elimu ilenge nini jamii inahitji Kwa muda huo!

Wazazi na jamii kuwa wachaguzi wa ndoto za watoto wao; baadhi ya wazazi huwachagulia watoto wao ndoto za maisha yao mfano utamkuta baba anamsisitiza mwanae “mwanangu mimi nataka uwe kama Mimi babayako ”hapa ni kwasababu baba kasoma udaktari na anaamini kuwa kitu pekee chenye kumsaidia mwanae ni kusomea udaktari.

Elimu kama hii haiwezi kuleta mabadiliko yeyote kwani mtoto alitakiwa kufanyia mazoezi kitu ambacho anakipenda na mwenye uwezo nacho .Kwa mifumo kama hii wataalamu wengi watakaozalishwa watakosa uwezo wakiutumishi kwani watakuwa na viwango duni ambavyo si sehemu ya uwezo wao kitaaluma .hivyo tutakuwa tumejidhulumu na kudhulumu jamii na taifa Kiu jumla Kwa kukosa watu bobezi kwenye taaluma zao .Wazazi na jamii wote Kwa pamoja wawe sehemu saidizi kwa watoto kutimiza ndoto zao nasiyo wachaguzi wa ndoto na njia wanazopaswa watoto wao kufuata .

Uhamasishaji mdogo kwa wagunduzi wa teknolojia mpya ;Bado serikali yetu inatakiwa kuongeza Uhamasishaji Kwa watu wenye uwezo wa kugundua teknolojia . Uhamasishaji huu usikike kupitia

Vyombo kamavile, runinga, magazeti,majarida.Lengo hasa ni kupata watu watakaoweza kuleta mabadiliko katika elimu yetu na uchumi wa kitanzania wagundizi hawa ndiyo watumike kama wakufunzi kwa wanajamii ili ujuzi huo uendelezwe kwa faida ya taifa letu hiyo ndiyo itakuwa elimu yenye Kuleta mabadiliko ya Moja Kwa Moja na siyo kubeza vitu vya kwetu nakuwa wategemezi na waamasishaji wa ujuzi wa kigeni .

Imejitahidi kuwapa motisha kidogo wagunduzi mfano picha happy chini inaonesha miundombinu ya umeme wa mgunduzi wa umeme “njombe

1.JPG

Picha hii imepatikana kwenye chanzo cha habari cha Azam​


Pamoja na yote bado serikali inahitaji kuendeleza elimu hii iwe ni moja ya ujuzi wa kivitendo zaidi

Wanafunzi Hulazimika kusoma masomo mengi yasiyo angalia uwezo wa wanafunzi kitaaluma; Kwa shule nyingi wanafunzi hupewa mzigo mzito wa kusoma masomo hadi kumi na kuyafanyia mitihani yenye kuwapima uelewa wao, japo baraza la mitihani huangalia masomo Saba tu , lakini pamoja na haya yote inatakiwa wanafunzi wapimwe kulingana na uwezo wao “subjects of their specialization” kwa kiingereza.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom