Mtz_D
New Member
- Jul 18, 2022
- 3
- 3
UTANGULIZI:
ELIMU ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga Akili, Tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi. Jamii hutumia Elimu kupitisha Maarifa, Ujuzi na Maadili kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine.
MAADILI ni mafundisho yanayotolewa katika nafasi mbalimbali hasa katika malezi, ili kuelekeza binadamu atende namna ambayo inamjenga yeye na jamii nzima.
Wakati tunapiga kelele juu ya upotevu wa fedha za serikali, kusuasua kwa miradi ya maendeleo, kukithiri kwa ubadhirifu wa mali za umma, pamoja na kukithiri kwa Rushwa kwa baadhi ya watumishi wa serikali, Je tulishawahi kujiuliza chanzo cha hayo yote ni nini ?.
Najua wengi wetu katika kulijibu swali hilo, tutakimbilia katika neno uadilifu, na tutasema kwamba baadhi ya watumishi wa serikalini ambao wameaminiwa na kupewa dhamana ya kusimamia majukumu fulani hawana uadilifu ndani mwao na ndio maana wanatanguliza maslahi yao binafsi mbele kuliko kutanguliza maslahi ya taifa letu kwanza. Tuko sahihi sana tukijibu swali hilo kwa kutumia neno uadilifu, lakini je tumeshawahi kujiuliza juu ya mambo yafuatayo ;
1. Ni wapi tumejifunza kuhusu huo uadilifu .
2. Ni wapi tumejifunza kuwa na uchungu juu ya taifa letu .
3. Ni wapi tumejifunza juu ya kulitumikia taifa letu kikamilifu .
Ni ukweli usiopingika kuwa, tukijiuliza kuhusu maswali hayo matatu, ni lazima tutapata ukakasi wa kuyajibu maswali hayo .
Tukiirejea maana ya Elimu, tutagundua kuwa msingi wa uadilifu kwa jamii yeyote ile ni Elimu, kwani jamii hutumia Elimu katika kupitisha maadili kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine. Hivyo ni dhahiri kuwa chanzo kikuu cha upotevu wa fedha za serikali, kusuasua kwa miradi ya maendeleo, kukithiri kwa rushwa pamoja na ubadhirifu wa mali za umma kwa baadhi ya watumishi wa serikali ni kukosekana kwa Elimu thabiti kwa wananchi wa taifa hili tokea wakiwa wadogo mpaka kufikia umri wa kulitumikia taifa hili kwa uchungu pamoja na nguvu zote.
Ndugu zangu katika kulijenga taifa letu, kupandisha uchumi wa nchi yetu, kudhibiti ufujaji wa rasilimali zilizopo ndani ya nchi yetu, tunahitaji kuwa na Elimu ambayo itatufundisha kuwa waadilifu, wazalendo wenye uchungu wa kulitumikia taifa letu lakini pia kutupa maarifa ya kuijua nchi yetu vizuri.
Sisi wenyewe ni mashahidi wa kwamba katika nyazifa mbalimbali kuna kanuni na sheria ambazo zinamuelekeza mtumishi wa serikali ni namna gani ya kutimiza majukumu yake ,lakini kwa kua hamna Elimu ya kutosha juu ya wajibu na uchungu wa kulitumikia taifa, wengi wa watu ambao wanapata nafasi ya kusimamia majukumu fulani huwa wanazichukulia sheria na kanuni mbalimbali kama ni sehemu tu ya vitisho vya kuwazuia kuweza kutimiza haja zao, Hivyo kupelekea kupuuzia sheria hizi pamoja na kanuni licha ya adhabu mbalimbali ambazo hutolewa juu ya wavunjifu wa sheria pamoja na kanuni hizo zilizowekwa.
Wengi miongoni mwetu tutagundua kuwa watu wengi katika taifa letu wamekuwa wakitafuta nafasi serikalini ili tu waweze kutimiza matakwa yao binafsi na wala sio kutimiza matakwa ya taifa , na ndio maana miradi mingi ya maendeleo imekua ikikwama na hata mingine kufa na kupotea kabisa.....
NINI KIFANYIKE
Taifa bora na lenye maendeleo ni lile ambalo daima lina watu ambao wana uchungu wa kulitumikia taifa lao kwa nguvu zote na kutamani maendeleo makubwa kwa taifa zima. Taifa ili liweze kusonga mbele linahitaji vijana watiifu, waadilifu, wanaoijua historia pamoja na malengo ya taifa lao kwa masiku yajayo na wenye ari kubwa ya kulitumikia taifa.
Hivyo basi katika mtaala wa Elimu yetu lianzishwe somo la "TANZANIA YETU", ambalo litafundisha ni wapi tanzania imetoka, ni wapi tanzania ilipo, ni wapi tanzania inaelekea na ni wapi Tanzania inataka kuwa, kwani kuanzishwa kwa somo hili kutasaidia vijana wengi ambao ndio nguvu kazi ya taifa kuwa na maono juu ya mustakabali wa taifa letu.
Somo hili la "TANZANIA YETU" lianze kufundishwa kuanzia Elimu ya msingi mpaka Elimu ya chuo kikuu bila ya kuwepo hiari ya kufanya uchaguzi wa kusoma somo hili. Kwa hakika somo hili litasaidia uadilifu kujijenga kwa vijana ambao ndio viongozi wa taifa la kesho lakini pia ndio nguvu kazi kubwa ya taifa na kuwafanya wananchi wote ndani ya taifa kuwa na uchungu wa kulitumikia taifa kikamilifu na kwa kujitoa.
Kama vijana wa taifa letu watapatiwa elimu ya kutosha juu ya kuwa waadilifu na wenye uchungu wa kulitumikia taifa lao tangu wakiwa watoto mpaka kufikia rika la utu uzima basi wataziheshimu sheria na kanuni zilizopo katika nyazifa mbalimbali na kupelekea taifa kuwa na watumishi Wakweli, Wachapakazi na Waaminifu.
FAIDA ZITAKAZOPATIKANA KUTOKA KATIKA SOMO HILI LA "TANZANIA YETU"
1. litasaidia kumjenga kifikra kijana na kumtayarisha kupambana na mambo mbalimbali hasa kwa lengo la kuilinda amani ya nchi.
2. litasaidia watanzania kuwa na umoja na mshikamano miongoni mwao kwa dhumuni la kulinda umoja na uhuru wa taifa.
3. litasaidia kuchochea ari ya kujituma kwa vijana, hivyo kupelekea kusimama kwa uchumi thabiti, kwani taifa lenye vijana wenye kujituma ndio taifa linalofikia maendeleo makubwa.
4. litasaidia watanzania kufahamu rasilimali za nchi yao kikamilifu hivyo kuzitumia kwa umakini mkubwa na hata kuzilinda dhidi ya wafujaji.
HITIMISHO:
Kwa kua Elimu ndio msingi wa kupitisha maadili kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine; Hivyo kama mfumo wetu wa Elimu utalenga kumfundisha kijana namna ya kuwa na maono juu ya mustakabali wa taifa, basi daima tutakuwa na watumishi wa serikali waadilifu, kama taifa tutakuwa na uchumi thabiti usiodorora bali kupanda lakina pia tutashuhudia maendeleo na mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali kama vile Kilimo, Siasa pamoja na Teknolojia hivyo kufanya watanzania wengi na kwa asilimia kubwa kuwa na hali nzuri ya kimaisha.
-----------------------------------ASANTE-----------------------------------------------------------

Upvote
3