Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
Siku Moja nilipokuwa nimetega sikio nikipata habari kutoka idhaa ya taifa nilivutiwa sana na Moja ya marudio ya usemi wa Baba wa taifa hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere ninanukuu, "Kama unadhani elimu ni gharama, basi jaribu ujinga".
Miaka mingi baada ya uneni huu lakini bado hakuna hatua za kutosha zilizotamba kuthibitisha majaribio ya aina ya elimu inayoweza kuushinda ujinga, mfumo wa elimu unaoweza kuudhibiti ujinga, lugha ya elimu inayoweza kuunyamazisha ujinga na sauti ya elimu inayoweza kusikilizwa na ujinga.
Inawezekana tunadhani tupo kwenye shabaha sahihi ya kuulenga ujinga kwa risasi zilizotoka nje ya utamaduni wetu lakini je, kuna utafiti wowote tulioufanya na kujiridhisha kwamba risasi hizo hazina madhara kwetu?
Kwanini tumekuwa wavivu kuwekeza nguvu,akili na fedha kuujaribu ujinga? Waingereza wana msemo wao kwamba kama haujafanya utafiti basi hauna haki ya kuongea, je sisi tumefanya utafiti gani kuhusiana na ujinga tulionao, aina ya ujinga, asili ya ujinga wetu, mazingira ya ujinga wetu, mbinu za kuuondoa ujinga wetu katika nia ile ile ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA!
Imekuwa rahisi sana kukumbuka simulizi ya KALIMANGENGA AKATAA SHULE lakini si rahisi kukumbuka kwanini alikataa shule?
Wengi waliokwenda shule wanadhani wamestaarabika hususani wakifanikiwa kukaa katika kiti ambacho mbele yake kuna meza ya keki ya taifa. Wala wasaza na kutupa mabaki jalalani, lakini wako wangapi kati ya wengi waliokwenda shule na kujimilikisha vyeti kabla ya kugeuka VIBARUA NAFUU WENYE VYETI.
Elimu yetu ingekuwa na tija zaidi endapo ingetupatia mwanga mkali wa kuumulika ujinga hivyo tangu zamani tungeshafanya utafiti wa kisayansi ili tupate kinyume chake. Hii ingetuepusha na hulka zinazonukia licha ya kutokuliwa hususani vyeti vingi bila ajira rasmi na zisizo rasmi.
Wakati kila mtoto akitamanishwa kujifunza ulimwengu mpya wa kiteknolojia na ubunifu huko Asia ya kati bado mtoto wa Mwaigomole anafundishwa kwamba asili ya binadamu ni nyani?
Bado anafundishwa historia ya utumwa, ukoloni na ubeberu lakini hafundishwi kitu kuhusu utumwa mbaya zaidi wa sisi vibarua wenye vyeti hivyo anaishi kwa kusoma kufaulu mitihani na siyo kufaulu mazingira yenye mitihani hata baada ya kuhitimu.
Juzi kwenye daladala nilipotoka Tegeta kurudi Ubungo nilikaa na Kijulanga mmoja aliyekuwa akisinzia kama pono sasa gafla gari liliyumba kidogo maeneo ya Lugalo pale akaamka gafla kisha akasema, "tuko wapi?" nikamjibu jifute kwanza matongo tongo tunakaribia Mwenge shida nini unalala ovyo hali bado U shababi wa taifa?
Akasema, "we acha tu nimechoka mno na mawazo tele, nina shahada ya biashara nimeajiriwa kwa Mchina mmoja tunasambaza friji. Ananilipa laki tatu kwa mwezi endapo nikitimiza shabaha ya mauzo ya shilingi milioni thelathini ambapo yeye katika mauzo hayo huingiza faida ya milioni SITA mpaka nane.
Natamani ningekuwana mtaji wangu mwenyewe lakini ndo ivo nina vyeti tu sikopesheki benki, bodi ya mikopo ya elimu ya juu wananidai milioni saba sasahuku Mwajiri wangu akinilipia 45,000/= kila mwezi. Hii inamaanisha kwamba inanichukua miaka 17 kumaliza deni.
Sasa huwa nawaza nitatoboa? Nimewahi kuomba ajira serikalini mara nyingi usaili unafanyikia Dodoma sasa nauli na malazi utakuta nakosa na siku nyingine nilienda nikakuta tupo watahiniwa 700 kwa nafasi saba ikimaanisha apatikane mtu mmoja katika watu 100 huu ni muujiza kwa kila aliyefanikiwa".
Nikamtizama Kijulanga yule kisha nikamwambia simulizi yako ni kama wewe ni Pwagu na Mimi ni Pwaguzi tumependa gari moja lakini nauli tutadaiwa kila mmoja ya kwake licha ya kuelekea kituo kimoja.
Kama ningepata fursa ya kuongea na washika dira ningenukuu biblia takatifu kitabu cha Mithali 15:31 "Sikio lisikilizalo lawama yenye uhai litakaa kati yao wenye hekim". Je, washika dira wapo tayari kusikiliza lawama hizi?
Washika dira wanatulaumu sisi kwamba siyo wabunifu lakini nasi tunawalaumu wao kwa kutunyima mfumo wa elimu yenye kutukuza ubunifu.
Ubunifu ni mchakato wa kutengeneza kitu kipya kitakachopelekea maisha bora zaidi ya yaliyopita na yaliyopo. Ni vigumu kwenda kinyume na kile tunachokisadiki lakini bila kufanya hivyo tutabuni nini?
Nguli wa sayansi Thomas Edison aligundua taa ya balbu ili aende kinyume na giza. Mwaka 1786 Alexander Graham Bell alikwenda kinyume na ufinyu wa mawasiliano nchini Marekani kabla ya kugundua simu.
Hata sasa katika ulimwengu wa kidigitali popo zangu mbili humuona tofauti bwenyenye wa dunia Elon Musk aliyejikita kwenye ubunifu wa magari yanayotumia umeme na kufanya uwekezaji mkubwa katika tafiti za sayari za mbali hususani mars na anga kwa ujumla. Je, tunadhani anapoteza bure pesa zake mtu huyu?
Alichotusaidia Walter Rodney mwaka 1972 ni kutueleza namna bara la Ulaya lilivyozorotesha maendeleo ya Afrika lakini pengine tungewahitaji kina Jenerali Ulimwengu wengi kuhuisha habari za kiuchunguzi na utafiti katika zama mpya.
Hii itatufanya hata tukifanikiwa kuwa wabunifu basi bidhaa zetu ziweze kukamata soko japo la ndani. Umewahi kujiuliza kwanini bidhaa za nje zinauzwa bei rahisi kuliko hizi za ndani?
Yaani sukari itengenezwe Brazil, isafirishwe kuletwa Tanzania, ilipiwe ushuru na tozo zote kisha isambazwe harafu bado iwe bei ndogo kuliko ile ya Morogoro?
Harafu baadae mshika dira anasema marufuku kuingiza sukari kutoka nje ili kulinda viwanda vya ndani, je hii ndiyo njia sahihi pekee ya kulinda ubunifu na uchumi wa ndani?
Lakini Mimi kibarua nafuu mwenye vyeti vingi nafahamu sababu ya taharuki hii. Bepari na kiwanda chake Brazil hutumia rasilimali watu wachache, teknolojia kubwa inayozuia upotevu wa malighafi na mzunguko wa miundombinu ya usafirishaji, mawasiliano na sera za rafiki za uwekezaji hivyo huzalisha sukari nyingi ndani ya muda mfupi lakini Mjasiriamali wa Morogoro kwake usafiri wa shida, vimeng'enyo vingi huagiza nje ya nchi, hutumia mashine za zamani zinazohitaji watu wengi, Kodi la serikali lukuki n.k
Sasa hapo ndipo tunatakiwa tuone namna ya kubadilisha mfumo wetu wa elimu na kupunguza orodha ya vibarua nafuu wenye vyeti katika maghala ya wageni wanaotumikishwa ujira mdogo.
Mfumo mpya wa elimu uzalishe Vijeba wanaong'amua mambo badala ya kuongeza Bei ya mafuta ya taa ili kuzuia uchakachuaji wa petroli kisha kuwaumiza wakulima wa pamba huko kijijini Mwamashimba Tabora basi waone Nuru ya kuwadhibiti wachakachuaji wenyewe.
Wacha niende kibaruani maana bwenyenye wangu hata nikiugua ananikata kiasi Cha fedha kwenye ujira wangu sembuse nikisema nilikuwa naandika makala?

Upvote
2