Elimu yetu tanzania

Elimu yetu tanzania

jafucha1992

New Member
Joined
May 8, 2013
Posts
1
Reaction score
1
Mimi ni mwanafunzi wa Dar es salaam Institute of Technology mwaka wa kwanza nachukua computer engineering.
lakini kuna kitu kimoja kinanisumbua kwanini wasomi wetu hawajulikani/hawatoi mchango katika jamii yetu .Kwa mfano mtu anachukua degree ya Agriculture lakini anapomaliza anaenda kutafuta kazi mjini badala ya kutumia maarifa aliyoyapata kwenda mashambani kufanya kilimo na mfano unamkuta mtu ana degree ya computer science afu hajawai kutengeneza hata software hata moja.Inashangaza,naitaji msaada wenu.
 
Elimu haikumuaandaa kujitegemea!zero confidence!
 
Hongera kwa kufika ulipo ILA soma ukimaliza utapata jibu kwa nn huwezi kurun hata software ya calculator au ya bili ya maji....(Elimu yetu ni elimu ya kuajiriwa na si kujiajiri)
 
ukweli Elimu yetu Tanzania imekwisha cjui baada ya miaka 20 ijayo tutakuwa wapi kwn ni suala la kushangaza kila siku elimu yetu inaporomoka toka shule ya Msingi mpk Vyuoni. ukiangalia sasa hivi wkuna baadhi ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na kuendelea na kidato cha kwanza wakiwa hawajui kusoma wala kuandika wala kusoma. hii yote ni kwa sababu serikali yetu haiko makini na suala zima la elimu hasa kwa kubadilisha mitaala pasipokuangalia madhara yatakayotokea baaada ya miaka kadhaa mbele. naiomba serikali iwe makini na jambo hili hata ikiwezekana iweke chujo toka shule za msingi kwa kuweka alama halisi za kupanda darasa. inasikitisha kweli na inauma watoto wanamaliza shule hawajui kusoma wala kuandika sijui walimu wanafanya kazi gani, pia nahisi sababu nyingine inasababishwa na walimu hasa waishio vijijini wanaoendekeza ulevi wakati wa kazi na hatimaye watoto wanabaki wanacheza kutwa nzima. hili ni jukumu la serikali kufanya uchunguzi na kulifanyia kazi jambo hili kwa ufanisi ili kuboresha elimu yetu la sivyo Elimu yetu itapoteza ufanisi wake.
 
Back
Top Bottom