Jana nimepata message nyingi watu wakita kujua kati ya KIPCHOGE na BOLT nani zaidi! hivyo leo ninaweka analysis kidogo kuhusu hawa wawili na nani ni mkali zaidi!
Usain Bolt wa Jamaica na Eliud Kipchoge wa East Africa ni wababe wawili wa kukimbia duniani. Bolt ambaya amestaafu karibuni alikuwa bingwa wa kukimbia mbio fupi aliyeweka record na pia Kipchoge wa East Africa ni bingwa wa marathion aliyeweka record hivi karibuni.
Usain Bolt’s record yake katika mita 100-ni at 9.58 seconds wakati Eliud Kipchoge’s record yake katika marathon ya ni 1:59:40.
Kama tukijaribu kufananisha hypothetically, kwa Usain Bolt kusustain same speed kwa mbio za marathon inamaanisha angeweza kumaliza marathon ndani ya 1:07:22 (Almost nusu ya muda wa KIPCHOGE)! Je hii inamaanisha nini? BOLT ni zaidi ya KIPCHOGE?
HAPANA Haimaanishi hivyo, Marathon is not all about super speed, but kusustain na kukimbia umbali mrefu tofauti na mbio fupi ambazo BOLT ameweka record. Kwa hiyo watu hawa wawili ni mabingwa katika mbio lakini huwezi sema yupi ni zaidi ya yupi. Kila mmoja ni mzuri katika umbali wake.
..