Elizabeth Michael (Lulu) kuachiwa Novemba mwaka huu?

Elizabeth Michael (Lulu) kuachiwa Novemba mwaka huu?

Decree Holder

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2015
Posts
2,559
Reaction score
3,745
Ikiwa Elizabeth Michael (Lulu) aliyehukumiwa miaka miwili gerezani kwa kosa la kuua atakuwa amepewa msamaha wa Rais Siku ya muungano tarehe 26/04/2018 kwa robo ya kifungo chake kama alivyopewa mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) basi atakuwa huru November mwaka huu.

Siku ya leo Joseph Mbilinyi (Mbunge) ameachiwa huru baada ya kuwa amepewa msamaha wa Rais kwa Robo ya kifungo chake, mashariti ya msamaha huo wa tarehe 26 April ni mtuhumiwa awe ametumikia robo ya kifungo chake baada ya kuwa amesamehewa 1/3 ya kifungo chake kama kawaida.

Lulu alihukumiwa miaka miwili gerezani Novemba 13 mwaka 2017 ambayo ni miezi 24. Ukitoa 1/3 anabaki na miezi 16 ya kukaa gerezani, mpaka Tarehe 26 April 2018 alikuwa ameshatumikia robo ya miezi 16 (kifungo chake), hivyo kama atakuwa ni mmoja wa wanufaika wa msamaha wa Rais akiwa amesamehewa 1/4 ya kifungo chake ambacho ni miezi 16, miezi anayotakiwa kukaa gerezani ni 12 tu ambayo inaisha Novemba 13 mwaka huu wa 2018

Take Note: Hii ni kama tu amepata msamaha wa Rais na si vinginevyo


UPDATES
Ameachiwa tarehe 12 May kwa amri ya mahakama atamalizia kifungo chake kwa kutumikia kifungo cha nje.

Msikilize N/Kamishina wa Magereza Tanzania
 
Na wenye makosa ya kuua msamaha unawahusu??
Rais anaweza kusamehe yeyote kama Babu Seya aliyehukumiwa maisha alipata msamaha pamoja na waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa kwa makosa ya mauaji walisamehewa hata Lulu anaweza kusamehewa
 
Na wenye makosa ya kuua msamaha unawahusu??
Rais anaweza kumsamehe mtu yeyote yule bila kujali kosa lake anayo mamlaka hayo...
Japo ni kweli kuna makosa hayana msamaha hasa ya mauaji,ubakaji,madawa ya kulevya, uporaji wa kutumia silaha za moto na mengine yanayo fanana na hayo.....
Lakini pamoja na hayo Katiba ina mpa mamlaka Rais kumsamehe yeyote yule bila kujali kosa japo mara nyingi wanao samehewa huwa wanakuwa ni wale ambao wameshatumikia kifungo husika au wana magonjwa fulani...
Hivyo inawezekana kabisa Lulu akasamehewa kabisa....
 
huyu dada wangemuacha tu amalizie kifungo chake atoke akiwa huru nafsi yake itatulia. Akitoka kwa msamaha hata kama alibakiza mwezi mmoja utawasikia tu wakianza kumsimanga. Bora amalizie tu miezi yake.
 
Msamaha wa Sugu doesn't count. Wameona aibu tu wakaona bora wamwachie. Magufuli ni dikteta uchwara .
 
akijibu nitagi
kuna mambo mawili
1.msamaha kwa wafungwa wote hupata msamaha wa ⅓ kwa mujibu wa sheria(katiba) isipokuwa wa kunyongwa maisha na wazuiwa!
2.msamaha wa rais ambao huwa ni ¹/6 hapa. kuna ambao hutoka kabisa na wengine hupunguziwa muda wa kukaa gerezan
 
Back
Top Bottom