Elon Musk ailaumu Twitter kukiuka makubaliano ya kuinunua kwa kutoa maelezo kuhusu idadi ya spam na fake accounts kama alivyoomba

Elon Musk ailaumu Twitter kukiuka makubaliano ya kuinunua kwa kutoa maelezo kuhusu idadi ya spam na fake accounts kama alivyoomba

babu M

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2010
Posts
5,222
Reaction score
3,173
Elon Musk ametuma barua ya malalamiko kwa Mkuu wa maswala ya kisheria wa Twitter akisema anaamini Twitter inakiuka merger agreement kwa kutotoa ushirikiano kuhusu idadi ya fake na spam akaunti kama alivyoomba.

Wakati wa makubaliano, Twitter alidai spam na fake akaunti zipo chini ya asilimia 5. Lakini siku za karibuni Elon amedai hiyo namba inaweza kuwa zaidi ya asilimia 20 na kuiandikia Twitter kutoa kwa kina namba zote za watumia.

Miezi michache iliyopita, Elon Musk alitoa ofa ya kununua kampuni yote ya Twitter kwa dola bilioni 44 ambayo ni sawa na dola 54 kwa hisa. Na pia walikubaliana kama Elon akivunja huo mkataba atatakiwa kuilipa Twitter dola bilioni moja.

Share za Twitter pre market zilikuwa zimeshuka kwa asilimia zaidi ya 5 na Tesla kupanda.
 
nilichokiona baada ya hili sakata Forbes huwa hawana data sahihi ya hizi pesa za hawa matajiri, kiuhalisia hizo pesa huwa hawana ni vile tu hukuzwa na media za magharibi
 
Back
Top Bottom