Elon Musk amerudi kuwa tajiri namba moja Duniani kwa mara nyingine tena

Elon Musk amerudi kuwa tajiri namba moja Duniani kwa mara nyingine tena

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Bwana Elon Musk ambae alikua Tajiri namba 1 Duniani toka August 2021 hadi October 2022 na kisha kua tajiri namba 2 kwa muda wa miezi 4 hivi kutokana na kushuka kwa thamani ya hisa zake, sasa amerejea tena kileleni.

Elon Musk aambaeni muanzilishi na mmiliki wa makampuni kadhaa ikiwemo Tesla, Starlink, Space X, Boring Company, Twitter, Neuralink, na mtandao unaokua kwa kasi ya ajabu wa OpenAl ama ChatGPT na nyingine nyingi.

Hisa zake zilishuka baada ya kununua mtandao wa Twitter na wabaya wake wakawa wanamponda na kumshambulia baada ya yeye kusema ataibadilisha twitter kua mtandao wa haki kwa wote. Hii ilipelekea kampuni yake ya Tesla hisa zake kupoteza ama kushuka thamani kwa karibu 65%.

Kwa vile elon ni akili kubwa, akawaacha wabaya wake wakabwabwaja weee kisha akaamua kuwapiga na kitu kizito kichwani, akashusha bei ya magari ya Tesla, baada ya hapo hisa zimepanda kwa kasi ya ajabu na kupelekea Elon kurudi kwenye nafasi yake ya Tajiri namba 1 Duniani.

Natamani Elon aendelee kua tajiri namba moja Duniani kwa miaka mingi sana.

 
Namkubali sana huyu jamaa.
FB_IMG_16740568451410123.jpg
 
Kuna waswahili wali shangilia huyo jamaa alipo tolewa namba moja ya utajiri duniani sijui wata semaje tena
 
Yaani huyo ndio Nape anakaza fuvu kwa kujizungusha kwenye mchakato wa kuiruhusu "starlink" itimbe bongo...🤔
Yaani huyu ndio Rostam anakaza fuvu kwa kamati ya roho mbaya ili asipewe vibali akiogopa ushindani na "starlink" isilete kazi zake bongo...🤥
 
Back
Top Bottom