- Source #1
- View Source #1
MADAI
Inadaiwa kuwa Tovuti ya Starlink inayomilikiwa na mfanyabiashara bilionea ambaye pia ni mmiliki wa Mtandao wa Twitter, Elon Musk imetangaza mpango wa kuleta huduma ya intaneti kwa njia ya satelaiti (starlink) nchini Tanzania kati ya Januari na Machi 2023 endapo itaruhusiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

- Tunachokijua
- Tovuti ya Starlink ya Elon Musk ina mpango wa kuleta huduma ya intaneti kwa njia ya satelaiti (starlink) nchini Tanzania
Katika kuthibitisha madai haya, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Jabiri Bakari alithibitisha kuwa ni kweli Kampuni hiyo ya Starlink ilituma maombi ya kuleta huduma ya Intaneti Tanzania.
Aidha kuhusu kuwasili kwa Starlink Corporation, Dk Bakari alijibu: "Ndiyo, ninafahamu kuwa kampuni hiyo ilituma maombi kupitia tovuti."
Mataifa pekee ya Kiafrika ambayo hadi sasa yameiruhusu Starlink kufanya kazi ni Nigeria na Msumbiji.
===
Pia soma: Mitandao ya simu ipige faida ya internet kwa mara ya mwisho. Elon Musk kuleta internet ya Starlink Tanzania