Elon Musk anatabiriwa kua Trilionea wa kwanza Duniani ifikapo 2027

Elon Musk anatabiriwa kua Trilionea wa kwanza Duniani ifikapo 2027

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Tajiri namba moja Duniani bwana Elon Musk anatabiriwa kua Trilionea wa kwanza Duniani mwaka 2027 kama utajiri wake utaendelea kukua kwa mwenendo unaokua kwa sasa.

Elon Musk utajiri wake unaongezeka kwa 110% kwa mwaka hivyo kama utakua hivyo ndani ya miaka 3 ijayo Elon atafikia hadhi ya kua Trilionea wa kwanza Duniani.

Trilioni 1 ya Marekani ni sawa na Trilioni 280 za Tanzania, sawa na bajeti ya Tanzania ya miaka 56.

Wengine waootarajiwa kua Trilionea ni kama ifuatavyo.
1. Elon 2027-110%
2. Adan 2028-123%.
3. Huang-2028
4. Prajogo-2028
5. Arnault-2030
6. Zuckerberg -2030
7. The Evil Genius -2030(Joking)

Soma hapa chini.
Elon Musk on pace to become world’s first trillionaire by 2027, report says Elon Musk on pace to become world’s first trillionaire by 2027, report says
 
He once was, and they still are

GettyImages-102371255-e1708949297235.jpg
 
Aje ainunue Tanzania iwe yake 🤣🤣 itabidi wadosi waanzishe haka ka utaratibu ka kununua nchi !

Nimeona report moja kwamba kwa sasa muhuni anamili asilimia 62% ya satelite zote angani mpaka sasa watu wanaanza kupata hofu kwa mtu mmoja kucontrol hayo makitu !! Atakua na ushawishi sana
 
hiyo 110% ni wastani wa ongezeko la utajari wake. Wastani.

ni ngumu sana kuwa trilionea haraka hivyo kwasababu performance ya makampuni haitabiriki

250b kwenda 1t itabidi aongeze 750b ndani ya miaka 3, uongo
 
Elon Musk anatarajiwa kuwa mtu wa kwanza duniani kuwa na $1,000,000,000,000 licha ya kuishi kwenye 'Nyumba ya Maboksi'.

Elon Musk yuko njiani kuwa trilioni wa kwanza duniani ifikapo 2027, kulingana na ripoti mpya ya utajiri wa ulimwengu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tesla kwa sasa ndiye mtu tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa dola bilioni 251, kama ilivyoripotiwa na Ripoti ya Bilionea ya Bloomberg.

Informa Connect Academy inafichua kuwa utajiri wa Musk unakua kwa kiwango cha kushangaza cha 110% kila mwaka. Ikiwa hali hii itaendelea, anaweza kufikia alama ya trilioni ya dola ndani ya miaka mitatu ijayo.

 
Hizi story za kusema, mtu tajiri anaishi kwenye nyumba ya "maboksi" Ni upuuzi tu, unafikiri ni maboksi kama haya ya bongo ya mateja wa magomeni!? Ni, mjengo haswa kama ikulu,
Kenge wengine utasikia, Eron musk, Jef Bezos, hawa wote ni "school dropout" Hawa kusoma! Waliishia njiani wakaacha shule wakaingia kwenye ujasiliamali! Sasa mburukenge wa bongo, anafikiri walikuwa wanasoma kama kwenye kayumba zetu, au, UDSM yetu, !
Mtu kama Bill Gates, wazazi wake walikuwa wanamiriki benk!sasa utasema alianza bila kitu, msingi ulikuwepo, ! Dangote, baba yake alikuwa anamiriki ndege, helkopta miaka hiyo ya 40s, 50s,
Acheni ujinga,
 
Nyumba ya bilionea Elon Musk.
 

Attachments

  • Screenshot_20240911-174259.jpg
    Screenshot_20240911-174259.jpg
    458.3 KB · Views: 18
Nyumba ya bilionea Elon Musk.
 

Attachments

  • Screenshot_20240911-174109.jpg
    Screenshot_20240911-174109.jpg
    467.5 KB · Views: 11
  • Screenshot_20240911-174030.jpg
    Screenshot_20240911-174030.jpg
    387.7 KB · Views: 11
Back
Top Bottom