Elon Musk anaunga mkono sana mapinduzi ya kijeshi yatokee Venezuela. Kuna siri gani nyuma ya hili?

Hata hivyo hizo sera zao zimeshindwa kufanya kazi, cuba iko wapi? Hata huyo maduro ni suala la muda tu, kwani misimamo yake sio kama ile ya mwanzo anachukua madaraka,
Sera kama zipi kwa mfano?
 
Wasingekuwa na mafuta wangeishi kaa amani kama Mongolia. Kosa lao ni kuwa na mafuta na kuwa karibu na USA.
Poleni sana Venezuela
Hilo hasa

Na watafanyaje? Wanataka wafanye juu chini wamtoe Maduro wamweke González waanze kuzitafuna natural resources za Venezuela
 
Hilo hasa

Na watafanyaje? Wanataka wafanye juu chini wamtoe Maduro wamweke González waanze kuzitafuna natural resources za Venezuela
Dollar value inafungamanishwa na Mafuta so inabidi mafuta mengi sana yawe chini ya milki ya USA ili dola yao isitetereke.

Mafuta kuwa chini ya uthibiti wa watu wengine wasio rafiki na USA inaweza sababisha yasiuzwe kwa dola na hivyo kuleta athari kwa thamani ya US dollar
 
Venezuela Maduro anatamba nini??? Ni aibu watu milioni sita wamekimbia nchi na wengi wapo Miami sababu Tu za Sera mbovu za Maduro? Maduro ana tofauti gani na Mugabe? Ni mambo ya aibu tu
 
Venezuela Maduro anatamba nini??? Ni aibu watu milioni sita wamekimbia nchi na wengi wapo Miami sababu Tu za Sera mbovu za Maduro? Maduro ana tofauti gani na Mugabe? Ni mambo ya aibu tu
Maduro ana sera mbovu kama zipi?
 
Maduro anA lipi? Ukiona 6 milioni citizens wamekimbia nchi ndo utamsifu Maduro? Hiyo ndo akili? Akili gani
Nilishalieleza hili kwenye message # 8

Lakini acha nilirudie tena kwa mapana na marefu.

Marekani walijaribu mara kadhaa kutumia CIA ili kuupindua utawala wa Maduro lakini wakashindwa na hawakuanza kwa Maduro tangu kipindi cha Chávez.

Baada ya mapinduzi kushindwa wakahamia kwenye vita vya kiuchumi.

Hii ilikuwa ni kipindi Obama akiwa raisi wa Marekani.

Sasa wangeanzaje kuiwekea Venezuela vikwazo?

Ikabidi watafute sababu za uongo:
  • Kwamba utawala wa Maduro unakandamiza demokrasia na lawama nyingine kibao kama unavyoijua Marekani kwenye figisu.
  • Serikali ya Marekani ikatangaza State of Emergency dhidi ya Venezuela, wakidai taifa hilo ni tishio kwa usalama wa Marekani. Ukisikia Marekani wanasema hivyo ujue hapo kinachofuata ni vikwazo vya kiuchumi walifanya hivyo kwa Iran na Syria pia.
  • Walianza kwa kutaifisha mali za viongozi wa Venezuela ambazo zilikuwa Marekani na Ulaya na hata baadhi ya viongozi wa Venezuela hawakuruhusiwa kuingia Marekani.
  • Hawakuishia tu hapo wakaweka vikwazo vikali vya kiuchumi ili kuigombanisha serikali na wananchi wa Venezuela. Kwa sababu walijua njaa ikiwa kali wananchi watafikiria kuipindua serikali.

Maana walijua kwenye vikwazo lazima hali mbaya ya kiuchumi itokee na kama ujuavyo uchumi wa Venezuela unategemea hasa exportation ya mafuta.
  • Vikwazo hivyo viliiondoa Venezuela katika mfumo wa biashara ya kimataifa

  • Venezuela ikaondewa katika nchi ambazo zingeweza kupata mikopo ya kimataifa kama ya IMF na WB
  • Huku Marekani ikitishia taasisi yoyote inayofanya biashara na makampuni ya Venezuela itawekewa vikwazo au kama ni kiongozi wa taasisi kifungo cha muda mrefu gerezani.

Matokeo yakawaje?
  1. Sekta ya mafuta ya Venezuela iliporomoka sana.
  2. Mapato ya nchi yalipungua kwa 99%
  3. Taifa la Venezuela likapata changamoto ya kuweza kununua bidhaa muhimu kama chakula, madawa n.k.
  4. Mfumuko wa bei ukawa mkubwa sana.

Kama ulivyosema hali hiyo ngumu ya maisha iliyosababishwa na vikwazo vya uchumi kutoka kwa Marekani ikafanya wananchi karibu milioni 7 kuhama nchi yao.

Baada ya Obama akaja Trump na Biden nao hawakuondoa vikwazo, wameendeleza State of Emergency iliyoachwa na Obama.

Ila Maduro kapambana angalau kwa sasa inflation imepungua kwa kiwango kikubwa sana.

Venezuela imekuwa ikiuza mafuta lakini kwa asilimia kubwa ni kwenye black market kwa China kwa sababu hairuhusiwi kutumia mfumo wa SWIFT ambao upo controlled na taasisi za kifedha za Marekani.

Marekani ni taifa la hovyo sana hapa duniani.
 
Nchi za kikomunisti zina viongozi kandamizi sana. Hakuna uhuru huko full manyanyaso.

Venezuela ni sawa na Tanzania ya CCM
 
Nchi za kikomunisti zina viongozi kandamizi sana. Hakuna uhuru huko full manyanyaso.

Venezuela ni sawa na Tanzania ya CCM
Ila Marekani ndio ina uhuru wa kutangaza mshindi wa uchaguzi wa Venezuela si ndio?

Blinken ana mamlaka gani ya kusema González ni mshindi badala ya Maduro kama alivyoandika kwenye huu waraka?

 
BREAKING: Venezuela inasema imezuia jaribio la mapinduzi lililoungwa mkono na Marekani na Spain, na kukamata silaha 400 za Marekani, na kuwakamata mamluki 14, akiwemo afisa wa kijeshi wa Marekani na raia 2 wa Hispania.
 
Like Mr. Musk, I think that the old, mediocre generation needs to be replaced, but I have included some East African nations in my list that also require political change.
 
Like Mr. Musk, I think that the old, mediocre generation needs to be replaced, but I have included some East African nations in my list that also require political change.
Do you support colour revolution attempts organized and run by USA in Venezuela?
 
Absolutely.

Even if they planned a comparable event in my country, I would fully support them.
Is it right for the US to intervene internal affairs in other sovereign states and society and decide who should be their leaders?
 
Is it right for the US to intervene internal affairs in other sovereign states and society and decide who should be their leaders?
With no shadow of doubt it is more than right, If we have leaders who misbehave and cannot be held accountable by their citizens, it is very very prudent for powerful nations like the US to intervene and bring back order.
Is it right for the US to intervene internal affairs in other sovereign states and society and decide who should be their leaders?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…