Elon Musk ataka Julius Malema apigwe vikwazo vya kimataifa na atangazwe kuwa mhalifu wa kivita

Elon Musk ataka Julius Malema apigwe vikwazo vya kimataifa na atangazwe kuwa mhalifu wa kivita

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Mjasiriamali bilionea Elon Musk ameibua mvutano mpya na kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF), Julius Malema, akipendekeza kwamba Malema atangazwe kuwa mhalifu wa kimataifa.

Mvutano huu umetokana na video ya Malema akidai kuwa chama cha Democratic Alliance (DA) kinawaunga mkono viongozi wake wa kizungu pekee, jambo ambalo Musk amepinga vikali.

Katika hotuba yake, Malema alisikika akisema:

"Hawa watu, ukitaka kuwagusa vilivyo, mpige mzungu. Wanaumia sana kwa sababu umemgusa mzungu. Si kwamba Mashaba na Solly hawataguswa, wataguswa, usijali. Lakini tunaanza na uzungu huu, tunakata koo la uzungu."

Musk amejibu kupitia mtandao wa kijamii X (zamani Twitter), akidai kuwa Malema anahamasisha mauaji ya Wazungu wa Afrika Kusini na hivyo anapaswa kupigwa marufuku kimataifa na kuwekwa chini ya vikwazo.

Soma pia: Trump atishia kusitisha misaada ya Marekani nchini Afrika Kusini kwa kunyakua ardhi kutoka kwa baadhi ya watu

Malema, kwa upande wake, amesema hawezi kutishwa na wito wa Musk wa kumwekea vikwazo na kumtaja bilionea huyo kuwa "mtoto aliyebembelezwa sana".

Musk.jpeg

Kiongozi huyo wa EFF amesisitiza kuwa ataendelea kutetea haki za watu weusi, hata kama hatua hiyo itawakasirisha viongozi wenye ushawishi katika jamii ya kimataifa.
 
Akina Malema hao ni wanafiki tu na hawana lolote kwani ni mara ngapi raia wa mataifa mbalimbali ya kiafrika waishio nchini humo wamenyanyaswa kwa kuporwa mali zao na wananchi wa Afrika Kusini hadi wengine kuuwawa na wala hawakulaani wala kuwapa fidia yoyote kwa mali zao zilizoporwa.

Malema bure kabisa.
 
Back
Top Bottom