Elon Musk ataka Radio Free Europe/Radio Liberty (RFE/RL) na Sauti ya Amerika (VOA) zifungwe akidai hazina umuhimu tena

Elon Musk ataka Radio Free Europe/Radio Liberty (RFE/RL) na Sauti ya Amerika (VOA) zifungwe akidai hazina umuhimu tena

Elon Musk ametaka kufungwa kwa Radio Free Europe/Radio Liberty (RFE/RL) na Voice of America (VOA), vyombo viwili vya habari vinavyofadhiliwa na serikali ya Marekani, akidai kuwa havina umuhimu tena.

Musk alitoa kauli hizi akijibu chapisho la Richard Grenell, Mjumbe Maalum wa Marekani, ambaye alikosoa vyombo hivyo kama vyombo vya habari vinavyofadhiliwa na walipa kodi, vikiwa vimejaa "wanaharakati wa siasa kali za kushoto."

"Ni vyombo vya habari vilivyomilikiwa na serikali," Grenell aliandika. "Vyombo hivi ni urithi wa zamani. Hatuwahitaji vyombo vya habari vinavyolipwa na serikali."

Musk alikubaliana, akituma ujumbe wa kusema: "Ndio, vifungiwe." Aliendelea kudai kuwa vyombo hivyo "ni watu wa siasa kali za kushoto wanavyozungumza na wenyewe huku wakiteketeza dola bilioni moja kwa mwaka za fedha za walipa kodi wa Marekani."
===================
Elon Musk has called for the shutdown of Radio Free Europe/Radio Liberty (RFE/RL) and Voice of America (VOA), two media organizations funded by the U.S. government, claiming they are no longer relevant.

Musk made the remarks in response to a post on X by Richard Grenell, the U.S. Special Envoy for Special Missions, who criticized the outlets as taxpayer-funded media filled with “far-left activists.”

“It’s state-owned media,” Grenell wrote. “These outlets are a relic of the past. We don’t need government-paid media outlets.”

Musk agreed, posting: “Yes, shut them down.” He went on to claim that the organizations “are just radical left crazy people talking to themselves while torching $1 billion a year of U.S. taxpayer money.”

Nafikiri VoA bado ni muhimu sana kwa muendelezo wa maslahi mapana ya Marekani hapa duniani. Chombo hiki wasikifunge kwa Sasa, ushawishi wao utapungua ghafla Sana hapa duniani na nchi hiyo kupoteza kabisa uungwaji mkono kutoka kwa jumuiya za Kimataifa.
Naamini MoD ya Marekani, CIA, FBI, na Taasisi zingine zote za Usalama za nchi hiyo zitalazimika kuingilia Kati na kumzuia Elon Musk na Mpango wake huo.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inaitegemea sana Taasisi hiyo katika kutekeleza majukumu yake hapa duniani.
Atusaidie na TBC yetu.

Hiyo Taasisi imekidhi Vigezo vyote kabisa vya kuweza kufutwa na kupotea katika uso wa dunia. Haina UMUHIMU tena kwa Tanzania hii ya Sasa. Kwa sasa hivi Taasisi hii imekuwa Kama Janga la kitaifa, haina faida tena kwa sasa kwa sababu imekuwa ikitumika vibaya sana na Watawala wachache Sana hapa Tanzania kwa ajili ya maslahi yao binafsi na Vibaraka wao. It's spreading the negative propaganda against the interest of the general public.
 
Mkuu VOA huwezi kuifuta kwa sababu una miliki X. Kwa national redio network hapo Marekani hakuna wa kiwafikia VOA na wapo mzigoni miaka zaidi ya 80 na wanatangaza kwa lugha zaidi ya 58 duniani kote. DOGE ni mpango wa kuilimiti Marekani na kuifanya kuwa week country.
MboNA China huo ugoro haupo na wanakimbiza kila nyanja,?
 
Umesema ukweli mtu,VOA ni chombo cha kipropaganda na ndio mana unaona ,kuna BBC swahili,Sauti ya Ujerumani,Radio france international,Redio Tehran,hivi vyombo ni kwaajili ya ujasusi labda kama hao jamaa wawili hawajielewi ila kuvifunga hivyo vyombo ni jambo la kuonyesha hawajui chochote kwenye mambo ya ujasusi.
Si jambo la kupepesa, wawili hao hawajielewi.
Hata USAID inayo sambaratishwa ni mpango wa kijasusi.
 
Kwa miaka mingi media zimekuwa ni njia ya Marekani na nchi za Magharibi kusambaza propaganda na ideologies zao

Kama wataamua kufanya hivyo kwa media na USAID, NED n.k sijui amejipangaje kwenye kusambaza propaganda na ideologies zao?

Mfano USAID ilikuwa ni moja ya taasisi ilibeba ushawishi mkubwa sana wa Marekani duniani

Ngoja tuone ndani ya hii miaka 4 ushawishi wa Marekani duniani utakuwa umepungua au kuongezeka.

Ni kama Marekani imetoa nafasi kwa mataifa mengine makubwa kutengeneza ushawishi
 
Hizi radio kwakweli hazina umuhimu sababu zinakupa habari za upande mmoja huku wakificha za upande wa pili...zifungwe tu
 
Trump anakuja kuleta mtikisiko mkubwa sana wa kiuchumi duniani ambao ni hatari sana kwa mataifa tegemezi.
Tunaelekea uelekeo wa ubabe/survival of the fittest, ukiwa mnyonge unamezwa.

Ni wakati wa GOT (Tanzania) wenye mamlaka kuanza kuchukua hatua ya kupambana na hili Kwa manufaa ya raia wake.
1. Serikali ianze kubana matumizi haraka sana
2. Serikali ianze kudeal na miradi yenye kuleta
return za haraka na huduma muhimu.
3. Serikali ianze kudhibiti mianya ya rushwa
haraka na Kwa nguvu kubwa sana.
4. Serikali ianze uwekezaji mkubwa kwenye
madini hasa Kwa wazawa small scale
miners,.
5. Serikali ianze kuwawezesha wakulima na
yenyewe inunue mazao kwa bei shindani na
kuweka stock kwenye maghala.
6. Serikali ipige marufuku madereva wa
bodaboda mitaani na kuwapa ajira jeshini
(JWTZ).
7. Serikali ianze kuencourage madereva wa
tax, bajaji wastaafu/wazee/akinamama/
vilema na wasioweza kufanya shughuli
nyingine za shuruba.
8. JWTZ ianze kuwa productive kwa kumiliki
mashamba makubwa sana ya mazao ya
chakula na viwanda vidogo vidogo vya
silaha na product nyingine ndogondogo.
9. Jeshi na majeshi yote yawe kwenye utayari
muda wote huku recruitment kubwa za
vijana wenye nguvu zikifanyika Kwa kasi.
10. Ni wakati wa Serikali kuanza kusimamia maadili sasa Kwa ukaribu na kupiga marufuku huu ujinga wote wa vijana mitandaoni na uchawauchawa, maana sasa tunakoendea jamii inahitaji watu serious wakuweza kukabiliana na uelekeo mpya wa Dunia ya ubabe, aka survival of the fittest.
 
Too late!
 
Kwa hiyo akina Ligongo, Mkamiti Kibayasi, Vincent Makoli hawa takuwa na kazi tena? Sitaki kuamini hili litatokea.
 
Kwa miaka mingi media zimekuwa ni njia ya Marekani na nchi za Magharibi kusambaza propaganda na ideologies zao

Kama wataamua kufanya hivyo kwa media na USAID, NED n.k sijui amejipangaje kwenye kusambaza propaganda na ideologies zao?

Mfano USAID ilikuwa ni moja ya sehemu ilibeba ushawishi mkubwa sana wa Marekani duniani

Ngoja tuone ndani ya hii miaka 4 ushawishi wa Marekani duniani utakuwa umepungua au kuongezeka.

Ni kama Marekani imetoa nafasi kwa mataifa mengine makubwa kutengeneza ushawishi
Propaganda na ideologies zipi zinazosambazwa na USAID, VoA, DW na BBC?
 
Back
Top Bottom