Elon Musk kuleta Intaneti ni tishio kwa mitandao ya simu, atapora wateja wenye matumizi makubwa na kuteka soko sehemu ambazo network inasumbua

Mi nashangaa sana eti hiv hii nchi sijui ipoje
 
Naombeni kujua starlink inafanyaje kazi ila pia hii mitandao yetu ya simu internet wanyotuuzia nao wanainunua kama ndio wanauziwa na nani kama hapana wao wanaitoa wapi kwa sababu najua wao hawana satellite zao angani
 
Inatumia satelite, limtambo lao lipo huko juu angani linaelea, wewe inahitaji ungo tu kunasa hiyo wifi yao
Kwahiyo hii internet inakuwa ni ukiwa nyumbani tu au ofisini? Vinginevyo mi na simu yangu popote ntaitumia vp wakati dish liko nyumbani au ofisini?
 
Tatizo mkuu ni Freemason ndo maana serikali yetu inasitasita inajua. Ni kwa faida yetu tusiingie kichwa kichwa tu. Maisha na Uhai wa mtanzania ni muhimu sana usiwekwe rehani eti kwasababu tu ya wazungu kuzuru na kuzuga huko mbugani. NASEMA HAPANA!
 
Egypt ni Africa lakini kielimu wako mbali tokea kale wasomi wengi walikuwa ndoto yao kufika Egypt kuchukua madini.
Misri wale wako mbali sana. Hata kilimo chao ni cha kisayansi sana na wanalima kwenye mazingira magumu. Ikija kwenye architecture wako njema sana. Angalia wanavyoi monitor na kuimudu Suez Canal moyo wa biashara ya logistics duniani?!
 
Hata kwenye simenti za dangote mlisema hivyo lakini haikushuka bei corruption is our great enemy tutabadilisha katiba na mitaala mashuleni na vyuoni lakini Kama tabia zetu na maalezi yetu hayatabadilika umaskini unakuja Kama jambazi
Bila hilo hii nchi ingekuwa mbali sana ila shida ni ubinafsi na ulafi wa viongozi na tumeifanya kuwa norm.

Yani mtu akiwa kiongozi asipokuwa mtu wa 10% na kuiba akiwa ofisini ili kujilimbikizia fedha na mali huwa tunamcheka na kumuona mshamba matokeo yake kila mtu anatamania kupata nafasi tu na kuanza kuiba serikalini.

Ukiwa mtu wa kupinga hizo tabia wanakuchukia utaitwa kiongozi mshamba na majina yote mabaya, watakuhujumu au hata kukuua ili waendelee kuiba kwa uhuru. RIP MAGUFULI.
 
Wanmchelewesha sio anachelewa. Kaomba vibali bado kimyaa... Halafu akina Mwigulu wanahaha ati wanatafuta wawekezaji na kuwapa motisha. Ndio mjue ccm inavyotutakia maisha mema. Kampuni hii ikija itasababisha hata hizi bando za kawaida kupungua bei
Huyo hawampi leseni, watazugisha documents sijui bla blaah...

Watamzungusha hadi akubali kuwapa % flani ya mgao halafu unakuta kwa mtu tajiri kama Musk hawezi ku deal na upumbavu wa aina hio. Tunaoumia ni sisi raia ila wanachokwepa ni ushindani. Natamani jamaa angeleta maombi enzi zile za jiwe angekuwa kashapewa leseni sio kwa huyu mbabaishaji waziri wa tweeter.
 

Ubaya wa hii nchi, viongozi wetu ni wafanyabiashara na hii inaleta mgongano wa kimaslahi ambao mara nyingi maamuzi yake huumiza wananchi.

Viongozi watu wa 10% sasa kampuni zinazotoa hizo percent ujio wa Elon Musk utaziumiza kwahio kete yao ni waziri kumkataa mwekezaji kupitia usumbufu wa kijinga wa document.
 
Ni sisi wananchi ndio tutapata maumivu kwa kuwa nyuma kiteknolojia, hao vigogo tayari washajivutia intenet ya mkonge unlimited majumbani kwao huku sisi wananchi bado tunanunua za kupimiwa MB / GB utadhani tunanunua ndonya za mchele
Waziri yeye ana unlimited ofisini, kwenye simu na nyumbani kwake.
 
Kwahiyo hii internet inakuwa ni ukiwa nyumbani tu au ofisini? Vinginevyo mi na simu yangu popote ntaitumia vp wakati dish liko nyumbani au ofisini?
Inafanya popote lilipo dish lako, as long as uko na dish lako hata kama unasafiri itafanya kazi
 
Umeonhea ukweli wanachelewesha makusudi hii bongo tutafika mbinguni hoi
 
Nitashangaa sana kama serikali itashirikiana na wamiliki wa makampuni ya simu kuzuia hii kitu kwa visingizio vya kodi au ajira za watu, waache market ifanye kazi yake na yakifa hayo makampuni ya simu kwa ajiri ya hii acha yafe tuu, yatazaliwa mengine maana mahitaji ya simu na internet yatakuwepo bado
 
Ushindani ni mzuri hata simu za mikononi zilishuka bei kwasababu ya ushindani. Tusiwe wepesi kukataa maendeleo ya teknologia kwa kohofia kodi. Je, tunakusanya kodi kiasi gani leo kwenye simu za nyumbani? zero.
Hiyo kitu ushindani sahau katika nchi ya kijima kama hii yetu,nchi ambayo karne ya 21 imepiga marufuku kitu kama paypal kwa sababu zisizoeleweka ndio waruhusu internet ya starlink halafu ije kuua kampuni zao walizoweka hisa!
 
MASHETANI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…