Elon Musk kuleta Intaneti ni tishio kwa mitandao ya simu, atapora wateja wenye matumizi makubwa na kuteka soko sehemu ambazo network inasumbua

Elon vibali kaomba Tanzania toka mwishoni mwa mwaka jana, anaambia habari za operational standards.

Rwanda wamechangamkia dili, wamempa licence tayari.
Inashangaza sana. Hivi ni standard gani hizo ambazo wanaona jamaa hana?
 
Kuna figisu nyingi sana zimeshaanza kuletwa na Vodacom Tanzania pamoja na Tigo

Hii nchi ina kampuni zenye kiburi sana
 
Napataje GB za bure kwa Tigo,Airtel au vodacom??
Njoo DM unifundishe.
 
Serikali ya mafisadi watakuja kusema
1) Hajatimiza vigezo na masharti
2) Ni hatari kwa usalama wa taifa
3) Ametumwa na mabeberu atuchunguze
 
Kuna figisu nyingi saba zimeshaanza kuletwa na Vodacom Tanzania pamoja na Tigo

Hii nchi ina kampuni zenye kiburi sana
Hizi kampuni hazina Huruma na mtanzania mnyonge, mbona Rwanda makampuni yapo na starlink yupo?, same to Mozambique?
 
Kuna figisu nyingi saba zimeshaanza kuletwa na Vodacom Tanzania pamoja na Tigo

Hii nchi ina kampuni zenye kiburi sana
Hawapendi kabisa kusikia hii kitu ambach kwao ni tishio. Sasa jiulize nani wanamiliki hizi kampuni?
 
Hivi unadhani kwanini Bei ya Bundle ni Gharama ? Jibu ni Serikali na TCRA kupenda mapato kwahio hata Starlink wasipokuja TCRA ikawaachia hawa mabwana wacheze na bei wanavyotaka Bei zitashuka (sababu bei zilikuwa chini kabla ya hao madubwana kuna na Bei Elekezi)

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…