Elon Musk kuleta Intaneti ni tishio kwa mitandao ya simu, atapora wateja wenye matumizi makubwa na kuteka soko sehemu ambazo network inasumbua

Elon Musk kuleta Intaneti ni tishio kwa mitandao ya simu, atapora wateja wenye matumizi makubwa na kuteka soko sehemu ambazo network inasumbua

Nadhani kuna masafa (frequency) ambazo watatakiwa kupewa ili kuweza ku access eneo hilo, ila kwa wale wa mipakani nadhani ni possible ku access huduma hiyo kutoka nchi wanazopakana!
Hapana , waulize canal plus serikali inaipinga ila hivyo visimbuzi vipo vya kutosha na mpira tunaona ......unadhani madishi ya starlink tutashindwa kununua??
 
Swali je nape na timu yake Voda Airtel tigo halotel Simba net watakubali hii kitu jibu ni hapana.
If they can't compete, let them join, NI dhambi kuifunga tanzania kwa namna hiyo, huduma hii itakapokuwa inafika kila pahala hata mapoorini itasaidia ku guarantee watalii huko Mbugani, wataweza kufanya lives touring huku wakionekana marekani na kwingineko duniani, WARUHUSIWE TU.
 
Hii ni dunia ya tekinolojia, katika ulimwengu wa biashara, tunasema huu ni ushindani (competition) katika biashara. Kwa wanaoelewa, hii wanaichukulia kama changamoto (challenge), na sio tatizo. Na bila ushindani hatuwezi kupiga hatua katika ubinifu (innovation). Tunaweza kuona nchi kama Japan wanavyoshindana kwa tekinolojia katika mechanics na electronics. Hivyo, makampuni yetu, yajipange kushindana na sio kuogopa tekinolojia mpya inayoingia. Maendeleo duniani yameletwa na mabadiliko ya tekinolojia. Niliwahi kusikia kuwa train ya mwanzo ilikuwa inatumia makaa ya mawe, lakini leo inatumia ninj? Hence, we shouldin't be resistant to changes, but responsive to changes.
 
Hata kwenye simenti za dangote mlisema hivyo lakini haikushuka bei corruption is our great enemy tutabadilisha katiba na mitaala mashuleni na vyuoni lakini Kama tabia zetu na maalezi yetu hayatabadilika umaskini unakuja Kama jambazi
 
faedf590-43a0-11ec-bf5e-027e37078eee


Bei ya vifaa vyote na kuwekewa ni shilingi laki 9.

kifurushi kinadumu kwa mwezi, nadhani anapanga bei kwa kuangalia uchumi wa nchi, Marekani ni 230,000/= , Nigeria ni 98,000, Hapa Kwetu si ajabu ikawa 70,000.

Ni internet ya kisasa, Speed yake ni kubwa sana, unaweza kushusha file la gb 1 speed ikiwa chini dakika 3 na speed ikiwa poa ni sekunde 50 tu, kwenye kuperuzi ni kugusa tu hakuna kusubiri, kucheki video ama video call hakuna mambo ya kuganda ganda.

Haina kikomo, ukitumia hata gb 20 kwa siku ni wewe.

Inaweza kupatikana mpaka mbugani, milimani, kwenye makorongo na sehemu remote ambazo mitandao ya simu haijaweza kufikia, Ni kama vile dstv.
.....................................................................................

ujio wake unaweza kupora wateja wengi wenye matumizi makubwa, hii ni hatari kwa makampuni ya simu na kama mjuavyo kuna watu wana hisa zao huko. Mbaya zaidi kifaa kimoja kinaweza kutumika hata kwa watu 50 kwa mpigo maana speed ni kubwa hata ikigawanywa, ni hatari ukizaliwa utamaduni wa watu kujichanga huku wakiacha kununua mabando,

Kwa kuwa internet ni ya Satelite hapa itaweza kufika hadi maporini na vijijini ambako maeneo hayo mengi internet huwa ni changamoto, hii itakuwa changamoto kwa mitandao ya simu hasa katika miji inayokuwa wakitaka kuweka minara watakuta tayari watu wameshazoea starlink.
..............................................................................

HITIMISHO

Kwa hali hii nadhani naanza kuelewa kwanini vibali vinacheleweshwa, sitashangaa njia ya kumuondosha ikiwa ni tozo nzito sana zitazofanya hata kifurushi kuwa bei mno ama tukaja sikia kisingizio kwamba huduma inaharibu mazingira, n.k.
Angalau sasa smart TV zetu zitapata kazi
 
Si yeye Bali huku kwetu. Wanahitaji mambo kadhaa kutoka kwake kabla hawajamruhusu kuingia soko letu. Ila kama anavyotueleza mleta mada, kuna watu wanachelea maslahi yao yatazimwa kwa ujio huu.
Elon vibali kaomba Tanzania toka mwishoni mwa mwaka jana, anaambia habari za operational standards.

Rwanda wamechangamkia dili, wamempa licence tayari.
 
Back
Top Bottom