Elon musk kuzindua huduma ya intaneti satellite ya Starlink nchini Uganda

Elon musk kuzindua huduma ya intaneti satellite ya Starlink nchini Uganda

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,386
Reaction score
2,833
1_20250426_175141_0000.png

Katika kuhakikisha Mtandao wa Starlink unazidi kushika Kasi ulimwenguni Tajiri Elon Musk ameamua kuongeza nguvu zaidi kwa kuleta huduma hii nchini Uganda.

Mtandao wa Starlink ambao unasifika kwa kutoa intaneti yenye Kasi na usio na wasiwasi Hatimaye wameomba leseni
Rasmi ya kufanya kazi nchini Uganda ikilenga kuleta mtandao wa intaneti wenye Kasi kupitia satellite katika Maeneo ambayo Yana changamoto ya mtandao au Serikali na Kampuni binafsi hawajafanikiwa kupeleka huduma.

2_20250426_175141_0001.png

Bado mawasiliano yanaendelea ili kuweza kukizi mahitaji dhabiti ambapo serikali ya Uganda inasema Kupitia Satellite hii Starlink itaweza kurahisisha mawasiliano ya kutumia intaneti kwa urahisi zaidi.

3_20250426_175141_0002.png

Japo huduma hii ilibidi kuanza kazi toka mwaka 2024, lakini ilicheleweshwa sasa itaanza Rasmi mwaka huu 2025, baadhi ya waganda Tayari wameshaanza kutumia huduma hii kupitia mfumo wa roaming service, lakini huduma kamili ya kitaifa inangoja kuidhinishwa rasmi.
 
Sehemu walizoanza kutoa huduma Kuna mabadiliko yoyote?

Mfano Kenya na nchi zingine?

Wananchi wao wanasemaje?
 
Sisi bado Serikali yetu inatulazimisha kununua vifurushi vya 1.4GB kutoka Vodacom/Airtel/Yass ambapo tunauziwa Kwa shilingi 3,000
 
Viongozi wa Tanzania ni kama vile hawajielewi
 
Sehemu walizoanza kutoa huduma Kuna mabadiliko yoyote?

Mfano Kenya na nchi zingine?

Wananchi wao wanasemaje?
Yap, ime force safaricom na wenzie washushe gharama ya vifurushi. Now internet services zinafika maeneo ambayo local SP hawafiki, na kwa speed kubwa
Ajira wise zimeongezeka, since vijana sasa wana access na internet, imekuwa rahis kwao kutengeneza online business without ku relocate kwenda miji mikuu

Hayo ni machache yaliyopo kenya
 
Gharama ya vifurushi vya huo mtandao wa Elon musk tafadhari, unaweza kushare tuone kwa hizo nchi
 
Bongo bado kupata internet ni ghali mno kulinganisha na majirani zetu, just imagine unapewa gbt 1 kila siku kwa mwezi mzima kwa 3000Frw tu.
 
Back
Top Bottom