Elon Musk ni kichomi

Sijaelewa rudia tena
Pesa wanadai zinapigwa na wamarekani wenyewe kwa miradi ambayo haina tija na mingine fake.
Ndiyo maana kama umefuatilia vyombo vya habari wanashangaa miradi iliyokuwa sponsored na USAID mfano dola milion 50 kwenda kununua condom gaza, dola milioni 200 kusaidia kilimu afghanistan sasa wanasema walikuwa wanasaidia kilimo cha zao linalotengeneza cocaine au maana ndicho kilimo kikubwa huko.
 
Na huku Bongo nyoso wamesema walikua wanazileta zije kufanya Kizimkazi Festival au hawajasema?
 
elon watamfukuza muda si mrefu, kwa sababu hana uwezo kuwepo serikalini, ni comedian na mfanyabiashara. umeona ile kuwachukia watu weusi alikotoka nao south africa, amesababisha hadi africa inyimwe misaada. mzungu yeyote aliyekuwa south miaka hiyo hadi leo hawapendi watu weusi, na kwa sababu trump hana nguvu kwake, atamtumia apendavyo.
 
... kabla nilikuwa nammaind sana Elon na hata kumhurumia, nikidhani ni Muafrica mwenzetu!
NAJUTA! 🤣
 
... kabla nilikuwa nammaind sana Elon na hata kumhurumia, nikidhani ni Muafrica mwenzetu!
NAJUTA! 🤣
baba yake na yeye akiwa mdogo sana, walikuwa ni matajiri wa south africa chini ya apartheid regime ambayo mwafrika hukutakiwa kuoga swimming pool moja na mzungu, kusoma shule moja, wala kwenda hotel moja. kama wazazi walikuwa hivyo yeye akiwa mdogo unafikiri hiyo mindset itakuwa imeondoka? ndio maana anachongea africa kwa trump. matajiri wa south wakitaka chochote marekani wanamwambia yeye, anatuchoma. south kuna sheria inataka ugawaji mashamba sawa na kwa weusi ili kuleta usawa, wazungu wameona hapa tufanyeje, wakampigia tu simu elon akasema kwa trump, na trump asivyokuwa na akili, ameenda moja kwa moja ati anaiwekea vikwazo soutth kwa sababu ya hiyo sheria. si sheria ya nchi, kwani ya mtu binafsi? ukiangalia vizuri, hata trump wamefanya makosa kumchagua, anaongozwa sana na hisia na ni rahisi kudanganyika.
 
Nyie acheni porojo nyingi zisizo na maana yoyote na unabii feki eti Trump atauawa, nyie nani kawambia wanataka kumuua.

Tatizo waafrika hamtaki kujishughulisha ili mjiondoe kwenye hili lindi la umaskini na ndio maana mnamlaumu Trump kwa kukata misaada.

Trump amechaguliwa na wamarekani na hao ndio wanapaswa waongee kumhusu na sio nyie na kama mnaona hamuwezi kuishi bila misaada basi nendeni mkawaombe China, Iran au Russia tuone kama watawapa chochote.
 
... KWAKWELI!
 
Nyie ndie wale watu wanaoionyaga Marekani BBC 🤣🤣. Kwa level za intel alizonazo Elon, pesa alizonazo, nguvu ya Ai alionayo, bado unadhani hajui analofanya??🤣🤣
... tumbafu ni tumbafu tu! pesa yake, nguvu yake, mavitabu aliyosoma na maroketi yake yanaweza kugeuka Kamba ya kumnyongea!
 
🤣🤣🤣🤣🤣. Nguvu yako inatikisa hata wilaya au kata yenu?...
Mwanzako hajui hata kama upo, dunia inamzungumzia.
... hata mke na Watoto wangu siwezi kuwatikisa!
Hapa tunaongelea jinsi mpumbavu mwenye mali anavyoweza kufanya makosa yakamgharimu! ... HISTORIA IMEJAA MIFANO!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…