Elon Musk ni mtu na nusu

Elon Musk ni mtu na nusu

Kwa hela hizo unahitaji mke wa nini? Una hela upangiwe utakula nini? Una hela ununiwe siku tatu? Una hela unyimwe unyumba? Una hela usipate mwanya wa kuongea na MTU yoyote wa jinsia ya kike hata Kama Ni dada yako?
Una hela upangiwe nguo za kuvaa?

Usituone sisi tusio na hela tumenyamaza, ukweli ni kwamba TUNAPITIA
Umenena vyema sanaaa
 
Habari JF

Huyu ni mtu na nusu, Yeah! Unaweza kusema hivyo. Elon Reeve Musk mapema wiki hii ameteka vichwa vya habari duniani baada ya kununua mtandao pendwa duniani( Twitter ) kwa dau la $44B, sawa na Trilioni 102.6 kwa pesa za kibongo.

Bilionea huyo namba moja duniani kutokana na takwimu za Forbes na Bloomberg, anakadiriwa kuwa na utajiri (net worth) wa $244B. Hii ina maana dili hilo la ununuzi wa Twitter limekunja takribani asilimia 18 ya utajiri wa Musk.

Elon hana shida na wala hafikirii jambo lolote baya kwenye ununuzi wake wa mtandao huo, kwani alishawahi sema kwenye moja ya kurasa zake za Twitter kuwa kumiliki mtandao huo ni moja kati ya ndoto zake, hivyo anaonekana yuko tayari kuingia costs zozote ili kuiishi ndoto yake.

Elon ni nani?
Kwa kifupi Elon Musk ni raia wa nchi tatu (Marekani, Canada na South Africa). Ameoa mara mbili na kuachika na ni baba wa watoto kumi pia. Ni mmiliki wa makampuni mbalimbali kama Tesla, PayPal, Space X nk.

Kwenye ukuaji wake Elon alipitia vipindi mbalimbali vigumu ikiwemo wazazi wake kutalikiana na hali ngumu ya kimaisha iliyokuwa ikiwakumba. Alianza ujasiriamali katika umri mdogo akishirikiana na kaka yake kwa kuuza bidhaa mbalimbali na kupitisha majumbani.

Alizaliwa South Africa kabla ya baadae kuhamia Canada kwa masomo ya chuo. Licha ya pia kufeli kuendelea na masomo hayo ya chuoni (discontinued). Baada ya kuwa drop out chuoni Elon aliamua kujikita zaidi kwenye biashara huku akipewa ushirikiano mkubwa na mkewe, na kwa shida na tabu Elon Musk alipambania kampuni zake zote mpaka kufikia hapo zilipo.

Mengine
Elon ni muumini mkubwa wa matumizi ya bangi, Na ni bilionea pekee alieweza kukuza utajiri wake kutoka $1B mpaka $244B ndani ya kipindi cha miaka 10.
Ukitaka kumvutia kijana wa kitanzania anzisha mijadala ya
1. Simba na Yanga
2. Sifa za matajiri na yupi ana fedha zaidi.
3. Kula tunda kimahasira.
 
Aliekuambia baba yake alishindwa kutoa huduma ni nani?

Huyu jamaa sio self made billionaire; baba take ana mchango mkubwa kwenye mafanikio yake.
Haya soma hapo mtanzania [emoji116]
Screenshot_20221029-102949-1.jpg
 
Kwa hela hizo unahitaji mke wa nini? Una hela upangiwe utakula nini? Una hela ununiwe siku tatu? Una hela unyimwe unyumba? Una hela usipate mwanya wa kuongea na MTU yoyote wa jinsia ya kike hata Kama Ni dada yako?
Una hela upangiwe nguo za kuvaa?

Usituone sisi tusio na hela tumenyamaza, ukweli ni kwamba TUNAPITIA

Sasa una hela kama Elon?
 
Kulingana na comment Yako Mimi sijui maana ya self-made.
Ndio maana nimekuomba unipe maana yake?
Nasubiri jibu ili nikaswaki
@Fursakibao ukipiga mswaki kunywa na chai kabisa, [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom