Elon ni genius sijawahi ona ulimwengu huu. Aliwekeza takribani dola milion 118 kwenye kampen za Trump ila ndani ya siku moja tu kapata dola billion 26

Elon ni genius sijawahi ona ulimwengu huu. Aliwekeza takribani dola milion 118 kwenye kampen za Trump ila ndani ya siku moja tu kapata dola billion 26

kali linux

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2017
Posts
2,192
Reaction score
5,685
Elon Musk ni kichwa sana yule jamaa.

Yeye ndie investor mkubwa kwenye rally ya Trump na inasemekena kwa ujumla aliwekeza dollar million 118.

Lakini baada ya Trump kushinda utajiri wa Elon ambae kwa sasa ndio tajiri namba moja umeongezeka kwa dollar billion 26 ongezeko hilo likitokana na kupanda kwa thamani ya hisa za makampuni yake jana baada ya ushindi wa Trump.

Ukiachana na ongezeko hilo la hisa elon anategemea kupata faida kibao kama ilivyoandikwa hapa na CNN https://edition.cnn.com/2024/11/06/business/elon-musk-election-bet/index.html
 
Pia kuna wanufaika wengine kwa upande wa soko la hisa kwenye ushindi wa trump kama ilivoandikwa hapa Trump’s victory adds record $64bn to wealth of richest top 10

Vile vile tumeshuhudia Bitcoin ikipaa zaidi, inategemewa kuvunja record ya usd 76,000 per BTC.

Stocks za makampuni yanayojihusisha moja kwa moja na AI kama NVIDIA nazo zimepaa sana baada ya ushindi wa Trump
 
Hawa sasa ndio wanufaika

Ukute sasa mtu yupo Magu ndani ndani huko toka asubuhi hajala wala mbuni hana mfukoni ila sasa povu linavyomtoka anachambua kampeni za urais marekani! Au anavyoichambua vita ya Israel na Iran.

Nilisahau, huyo mtu unakuta hata kuoga hajaoga na hata kazi hana anashinda kijiweni tu
 
Polepole chief

Kwa wengine hio nayo ni burudani, uchambuzi na soga khs mambo kama haya kwa wengine ni burudani pia.
 
Huyu jamaa kwenye kampeni za trump alikua anaruka ruka kama mtoto jukwaani, he was totally invested in it.
Matajiri wa hadhi yake wanajulikana kwa utulivu wa hali ya juu sana, wasioonesha hisia, msisimko wala fukuto lolote.

Sasa ukiona mpaka kibosire kama yeye anaruka vile na kusimamia kampeni, wewe jua mkeka wake tayari alishauona uleee unatiki kama alivyopanga. Famasikhara, nini?
 
Ila Huyu jamaa haiba yake yakipekee sana.

Unajua kule twitter hata kabla ya kuinunua alikuaga anajibu kila mtu kwenye tweets zake, na yupo online muda mwingi, na hapo anasimamia makampuni almost sita
 
Ila Huyu jamaa haiba yake yakipekee sana.

Unajua kule twitter hata kabla ya kuinunua alikuaga anajibu kila mtu kwenye tweets zake, na yupo online muda mwingi, na hapo anasimamia makampuni almost sita
Ila una hakika ni yeye binafsi Elon? Tuko katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia. Halafu, anaweza kuwa na mafundi wa kumfanyia kazi kama hizo, yeye akaenda kujibanza Los Angeles kwenye SpaceX yake, nk.
 
Back
Top Bottom