Nafikiri ni muhimu kama mzazi ukaongea na huyo mtoto ili kubaini ni kwa nini huwa anaomba kiasi hicho cha pesa na si zaidi wala pungufu-hii itakusaidia kubaini matumizi ya mtoto na kutambua vipaumbele vyake ktk matumizi ya pesa!Hili ni muhimu kwako mzazi bila kujali kuwa mtoto ni wa kike au wa kiume!
Mkuu kindafu,
Thanks much kwa mawazo mazuri, na wengine wote bila kukusahau 'Mzee' kwa na mchango wako hapo juu.
Inshu ni kwamba mtoto ni wa class II na anasomea shule nzuri tu English Medium ambapo kimsingi naweza sema anapata huduma karibu zote muhimu kuanzia usafiri wa school bus kwa kwenda na kurudi kutoka shuleni, breakfast, pamoja na lunch kabla ya kurudishwa nyumbani mchana, japo shule yenyewe ni ya kutwa.
Sasa ni ukweli kabisa kwamba mimi kama mzazi nilijaribu kufanya udadisi kwa mtoto ili kupata kufahamu hiyo pesa anayoombaga huwa ni ya matumizi yepi ya ziada, na ni kwa nini anaombaga sh. 200/- tu na si zaidi kama jinsi na ninyi mlivojaribu ku'raise concern wakuu.
Sasa baada ya kufanya udadisi nlichokuja gundua ni kuwa ile breakfast itolewayo shuleni ninayoilipia kwa term in advance kumbe huwa ni uji pekee bila kitafunwa chochote, japo uji wenyewe ni ule wenye mchanganyiko wa virutubisho, ambao hujulikana maarufu kama 'uji wa ulezi'!
Na nilipoendelea kudadisi zaidi ndipo pia nikagundua ya kwamba, tofauti na jinsi nilivyoielewa mimi ile dhana ya kwamba ni 'strictly prohibited kwa mzazi yeyote kumfungashia mtoto wake chakula cha ziada kutoka nyumbani (cuz, at least that was one of the school's general rules of admission), kumbe pale kwenye school compound huwa kuna kiduka ambacho, aidha ni mradi wa shule (au mradi wa waalimu maybe) ambako ndiko watoto huuziwaga vitafunwa ifikapo muda wa breakfast; yani kwa mana hii ni kwamba, kumbe wakati wengine wanakunywa uji bila vitafunwa, kuna watoto wengine huwa wanakunywa uji na vitafunwa according to sizes of their pockets!
So, tofauti ya kimtazamo inayojitokeza sasa kati yangu mimi na wife wangu ni kuwa, wakati mimi naona ni kumtendea haki mtoto wangu ili asijiskie unyonge na au kutamani watoto wenzie wanapokula good-time, wife wangu yeye anaamini ya kwamba shule ilikuwa na maana nzuri sana ku'provide breakfast ya uji pekee bila vitafunwa kwa watoto wote ili kuleta usawa (uniformity) katika uvaaji, ulaji n.k, na kwa maana hiyo mimi kumpatia mtoto pocket money kwa ajili ya vitafunwa n.k ni kumfundisha mtoto tabia mbaya sana, sasa hii sijui mnaona imekaaje wakuu, maana kwa upande mngine naona wife nae kama ana ka'point' flan vile ... ??
Nawasilisha.