Emanuel Nkulila's song: Pain in Me

Pain in me imenikumbusha kitambo sana. Miaka ya 2000s mwanzoni. Enzi hizo nasikiliza kipindi cha chombeza time Radio one, sijui bado kipo hiki kipindi na makali yake yako kama zamani?
 
2003 kuna sehemu anapenda sana kuja hapo maeneo ya moshi nilishamkuta kama zaidi ya mara 4 sijui ndugu zake au huyu jamaa katokea mkoa gani
 
Nkulila ni mwanamuziki mzuri aliyebobea sana katika muziki, nadhani kasomea Muziki. Nyimbo zake zote nilizowahi kusikia zimetungwa vizuri sana, ila yeye mwenyewe siyo mwimbaji mzuri; nadhani aliwekeza zaidi katika music composition na arrangement kuliko vocals zake. Wanamuziki vijana wetu wa leo wangemtumia kuwasaidia katika kupangilia nyimbo zao wangetisha sana Afrika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…