Baada ya kuishi nao hasa kule Kanda maalum niligundua yafuatayo, Wanaume wao ni majasiri Sana, mwanaume wa kijaluo kwanza ana wivu na mke wake, iyo ipo Kwa kila mwanaume rijali, pili Mwanaume wa kijaluo qnapenda Sana familiya yake, Wanaume wa kijaluo wanajipenda Sana ..Wanaume wa kijaluo hawapendi kutawaliwa tawaliwa kiboya, Wanapenda kusifiwa....hasa nyakati wakiwa na pesa mingi.
Wanaume wa kijaluo Wanapenda kuabudiwa na jamii yake hasa akiwa na pesa.
Wanaume wa kijaluo hawaogopi.
Wanaume wa kijaluo Wanapenda Sana miziki Yao.
Wanaume wa kijaluo Wanapenda kula vizuri vyote...
Kwenye maswala ya kutahiriwa jamaa siku hizi Wanapenda Sana SaRO(Jando) na hii kutokana na hali alisi ya usasa juu ya magonjwa yanayoweza kuambukizwa Kwa njia ya kujaamiana, pili inakuwa ni aibu Kwa vijana wasiopitia hiyo steg, nakumbuka Kuna miezi kadhaa vijana wanakusanyika Wanapenda kufanyiwa tohara sehemu mahalum,Kisha wanafanyiwa sherehe ..na huu utamaduni umekuwa baada ya kuanzia kuoleana Kati ya kabila mbili Luo na Kurya, mwisho wa siku wamepeana na kubadilishana Sana tamaduni.
Swala la kuridhiana wanawake...ni kweli hilo lipo, nasiyo Kwa waluo tu ,bali Kwa makabila mengi Sana apa nchini, Kwa mfano uko pwani, kusini mwa Tanzania na hata baadhi ya mikoa ya Kanda ya ziwa...hata Kurya pia ufanya hizo Mila ...