Emerald hotel Zanzibari, kwa sasa ni The Mora Zanzibar hotel

Emerald hotel Zanzibari, kwa sasa ni The Mora Zanzibar hotel

kama mwanahabari mkongwe unaefahamu misingi ya uandishi na weledi wake, unafahamu vizuri sana mahali pakupata ufahamu, uelewa au ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali serikalini 🐒

hii kubabaika na wasiwasi ambayo si muhimu umeibebea wap na umeanza lini ndrugu kutaka kuleta taharuki kwa Jamii EMANUEL misalaba
Mkuu Tlaatlaah Je hadi hapo umeshajibu maswali yangu?
 
kama mwanahabari mkongwe unaefahamu misingi ya uandishi na weledi wake, unafahamu vizuri sana mahali pakupata ufahamu, uelewa au ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali serikalini 🐒

hii kubabaika na wasiwasi ambayo si muhimu umeibebea wap na umeanza lini ndrugu kutaka kuleta taharuki kwa Jamii EMANUEL misalaba
Tlaatlaah mimi ni raia, mlipa kodi na mpiga kura wa kawaida wa huku shamba ya baina ya Charawe na Ukongoroni.
Maswali yangu naona hujayajibu mkuu.
 
Sasa mbona wauliza maswali yako mahali ambapo sio sahihi...

Majibu ya maswali yako wanayo hao unaowaita mawaziri...
 
Wana Jf habari za kutwa nzima ya leo wakuu!

Wadau kuna kitu hapa sielewi natamani wajuzi wanisaidie huenda hofu na mashaka vikaniondoka.

Wiki hii tangu ianze 04/03/2024, hadi siku ya leo 08/03/2024, imekuwa ni wiki ya u busy sana wa misafara ya kila mara ikitoka na kuingia si asubuhi, si mchana wala jioni na hata usiku misafara bandika bandua, huko Emerald hotel Zanzibari kwa sasa ikijulikana The Mora hotel iliyoko katika ufukwe wa Matemwe Muyuni kaskazini mwa Kisiwa cha Unguja.

Misafara hiyo inahusisha magari ya SMT na SMZ, katika kudadisi ni baadhi ya mawaziri wakifanya vikao na Wamarekani hapo hotelini kwa karibu siku 5 na kesho Wamarekani nimejuzwa wataondoka.

Maswali yangu ni.

1. Kwa misafara hii ya kila siku ikihusisha magari ya serikali ambayo huendeshwa na kodi za wananchi.

Nimejitahidi kutafuta kwenye Vyombo mbalimbali vya habari kuona vikao hivi labda vimeripotiwa na vyombo vyetu vya habari, lakini sijaona kabisa,
Kwa nini vikao hivi vimefanyika kwa siku zote hizi bila ya kuripotiwa na vyombo vya habari?

2. Je au mimi nimepitwa na taarifa za habari kuhusu hii mikutano?

3. Kama ni vikao vya viongozi wetu vya kibinafsi na hao Wamarekani, je wako sahihi kutumika misafara mikubwa ya kiserikali vile halafu bila kuripotiwa?

4. Si lazima waseme wamejadili nini bali ni vikao vinahusu nini.

5. Wanajidili nini ambacho hawataki kuujulisha umma?
Natanguliza shukurani.
kwani usiende hapo ukawaulize?
 
Tlaatlaah mimi ni raia, mlipa kodi na mpiga kura wa kawaida wa huku shamba ya baina ya Charawe na Ukongoroni.
Maswali yangu naona hujayajibu mkuu.
bas sawa,
vuta subra kidogo, bilashaka umewakilisha wengi ambao pia labda wangependa kufahamu kinachoendelea japo ni kazi za kawaida tu za kila siku...

kwa wakati muafaka ikionekana inafaa basi wahusika wataeleza kinagaubaga kinachoendelea na moyo wako na wengine ipate kutulia 🐒🐒
 
Shukurani sana mkuu
 
Back
Top Bottom