Emerging Stars ya Kenya imeanza vyema kampeni yake ya kufuzu AFCON U23 2027 baada ya kuishinda Taifa Rising Stars ya Tanzania kwa mabao 4–1 katika mchezo wa raundi ya kwanza uliochezwa Nyayo Stadium Jijini Nairobi.
Kenya ilipata mabao kupitia Paul Osama, Lawrence Okoth, Kevin Wangaya na Kelly Madada, huku Tanzania ikipata bao moja la kufutia machozi kupitia penati ya iliyochongwa na Sheikhan Khamis.
Matokeo hayo yanaipa Kenya faida kubwa kuelekea mchezo wa marudiano nchini Tanzania Jumanne wiki ijayo, Jijini Dar Es Salaam.
Lakini huu si ushindi wa kawaida tu wa mechi moja. Ni pambano la timu za vijana kutoka nchi mbili ambazo zimekuwa zikishindana mara kwa mara katika soka la Afrika Mashariki, na safari hii Kenya imepata nafasi nzuri ya kusonga mbele.
Mshindi wa jumla wa michezo yote miwili ataendelea na raundi inayofuata ya mchujo, ambako Côte d’Ivoire inasubiri.
Je, 4–1 ni pengo kubwa sana kulifunga kwenye mchezo wa marudiano, au bado Tanzania inaweza kufanya comeback mbele ya mashabiki wake nyumbani?
Na kwa Wakenya, Je Emerging Stars wanaonesha dalili za kizazi kipya cha Harambee Stars, au bado ni mapema kutoa hitimisho kutokana na mechi moja?