JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
"Kama tukiambiwa kusimamisha safari tutafanya hivyo, lakini kwa sasa kila kitu kinaendelea kama kawaida," - Sir Tim Clarke.
Makampuni mengi makubwa ya ndege yalisitisha safari zao kwenda Urusi baada ya taifa hilo kuwekewa vikwazo kwa kuivama Ukraine kijeshi.
Ndege za Emirates ni kati ya chache ambazo bado zinaendelea na safari kuelekea Moscow na St Petersburg.
Sir Tim ameongeza kuwa inatakiwa kufahamika watu wa Urusi wao siyo wahusika wakuu na maamuzi ya vita ya Ukraine.
Source: BBC