Rais wa Emirates, Sir Tim Clarke amekataa kufuata agizo la Nchi za Ulaya kuiwekea vikwazo Urusi kwa kusitisha ndege kwenda Nchini humo, akisema hayo maamuzi yanatakiwa kufanywa na Serikali ya United Arab Emirates (UAE)
"Kama tukiambiwa kusimamisha safari tutafanya hivyo, lakini kwa sasa kila kitu kinaendelea kama kawaida," - Sir Tim Clarke.
Makampuni mengi makubwa ya ndege yalisitisha safari zao kwenda Urusi baada ya taifa hilo kuwekewa vikwazo kwa kuivama Ukraine kijeshi.
Ndege za Emirates ni kati ya chache ambazo bado zinaendelea na safari kuelekea Moscow na St Petersburg.
Sir Tim ameongeza kuwa inatakiwa kufahamika watu wa Urusi wao siyo wahusika wakuu na maamuzi ya vita ya Ukraine.
View attachment 2191982
Source: BBC