KWELI Emmanuel Ntobi amevuliwa uongozi uenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga

KWELI Emmanuel Ntobi amevuliwa uongozi uenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Wakuu naomba msaada wa taarifa hii kuwa Kamati tendaji ya Kanda ya Serengeti imefikia maamuzi ya kumvua Uongozi Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Bw. Emmanuel Ntobi kutokana na utovu wa nidhamu na maadili ikiwemo kuchafua Viongozi wa Chama chake Kitaifa kupitia mitandao ya Kijamii.
Screenshot 2025-01-09 100034.png
 
Tunachokijua
Emmanuel Ntobi mwaka 2024 alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa wa Shinyanga, kabla ya hapo Ntobi aliwahi kuwa mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Shinyanga kabla ya mwaka 2023 kuondolewa katika kiti hicho kwa madai ya vitendo vya utovu wa nidhamu.

Kuelekea Uchaguzi wa viongozi ngazi ya taifa ndani ya chama hicho Ntobi amkuwa na mtazamo tofauti hasa dhidi ya wagombea wa nafasi ya uenyekiti ambapo ameonesha kuunga mkono Freeman Mbowe huku akidaiwa kutoa kauli zisizo za kinidhamu kupitia mitandao ya kijamii dhidi ya Tundu Lissu aambaye pia ni mgombea katika nafasi hiyo.

Kumekuwapo na taarifa inayosambaa mtandaoni kuwa Emmanuel Ntobi amevuliwa uenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga.


Je ni upi uhalisia wa taaifa hiyo?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa ni kweli Emmanuel Ntobi amevuliwa uongozi nafasi ya uenyekiti CHADEMA mkoa wa Shinyanga kupitia kikao cha Kamati tendaji ya Kanda ya Serengeti kilichofanyika Januari 8, 2025, Shinyanga Mjini.

Katika kutafuta ukweli wa taarifa hiyo JamiiCheck ilimtafuta Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika ambaye alisema “Naomba wasiliana na Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti au Katibu wake kwa kuwa maamuzi hayo ni ya Kanda ya Serengeti na wao ndio watakaosema kama ni taarifa sahihi au sio sahihi.”

Aidha JamiiCheck imemtafuta mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti (CHADEMA), Lucas Ngoto ambaye amethibitisha juu ya taarifa ya kuvuliwa kwa uongozi wa chama hicho Emmanuel Ntobi mkoa wa Shinyanga huku akisema hawajamkabidhi barua rasmi licha ya maamuzi kutolewa.

“Ni taarifa ya kweli, kikao kilifanyika Januari 8, 2025, Shinyanga Mjini, alipewa nafasi ya kujitetea, akatakiwa kuondoka kwenye kikao baada ya hapo ili maamuzi yafanyike ndipo taratibu za maamuzi zikaendelea.

“Maamuzi yameshafanyika, Ofisi ya Katibu inaandaa barua ili imjulishe maamuzi ya kikao, bado hajakabidhiwa majibu rasmi licha ya kuwa maamuzi yameshatoka.”


Hata hivyo kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii, za CHADEMA kanda ya Serengeti imechapishwa taarifa inayouhabarisha umma juu ya kuvuliwa kwa uongozi wa Ntobi ndani ya chama hicho.

Awali, Desemba 26, 2024, wajumbe wa Chama hicho mkoa wa Shinyanga walionesha pia kupingana na Kauli yake iliyodai Mkoa huo unamuunga Mkono Freeman Mbowe kwenye Kinyang'anyiro cha Kugombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa, hali inayoonesha kutokuwepo kwa maelewano baina yao kwa muda mrefu.​
Back
Top Bottom