Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Shinyanga Emmanuel Ntobi amesema uamuzi uliofikiwa na kamati si sahihi kutokana na kushindwa kufuata taratibu, kanuni na katiba iliyowekwa na chama hicho.
Ntobi ameeleza hayo wakati akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa Wasafi FM ambapo amenukuliwa akisema:
“Sababu kubwa ni joto la kisiasa linaloendelea kwenye chama chetu, niseme tu kuwa nimeonewa kwasababu tu namuunga mkono Mhe. Freeman Mbowe kuelekea kwenye uchaguzi wa viongozi wa chama chetu.
"Hatua za kinidhamu zilizochukuliwa hazijafuata utaratibu kulingana na katiba ya chama chetu, wanapaswa kuniingiza kwenye kamati ya maadili kwa tuhuma zinazonikabili, sijatukana kiongozi yeyote bali ni maoni tu niliyotoa mtandaoni” amesema Ntobi.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2023 Ntobi aliwahi kusimamishwa Uenyekiti wake kwa mwaka mmoja kutokana na makosa ya kinidhamu.
Ntobi hivi karibuni maekuwa akilalamikiwa kwa baadhi ya maandiko na kauli zake dhidi ya Mgombea wa Uenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu