Pre GE2025 Emmanuel Ntobi: Nimeonewa kwa sababu namuunga mkono Mbowe kwenye Uchaguzi wa chama chetu

Pre GE2025 Emmanuel Ntobi: Nimeonewa kwa sababu namuunga mkono Mbowe kwenye Uchaguzi wa chama chetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakianza kuwajibishana kwa kusingizia matusi wasije kushangaa serikali itakapokuwa inawawajibisha kwa kisingizio hicho hicho. Wapinzani uchwara.
 
YEricko mavitabu

1000314656.jpg
 
Endapo lisu yupo fiti kiasi cha kumsimanisha mtu wa mbowe basi ujue lisu si wa mchezo mchezo
 
“Sababu kubwa ni joto la kisiasa linaloendelea kwenye chama chetu, niseme tu kuwa nimeonewa kwasababu tu namuunga mkono Mhe. Freeman Mbowe kuelekea kwenye uchaguzi wa viongozi wa chama chetu.
Kwahiyo ameondolewa na wafuasi wa Lissu
Huu ni mpasuko wa pili ndani ya chama
 
Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Shinyanga Emmanuel Ntobi amesema uamuzi uliofikiwa na kamati si sahihi kutokana na kushindwa kufuata taratibu, kanuni na katiba iliyowekwa na chama hicho.

Ntobi ameeleza hayo wakati akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa Wasafi FM ambapo amenukuliwa akisema:

“Sababu kubwa ni joto la kisiasa linaloendelea kwenye chama chetu, niseme tu kuwa nimeonewa kwasababu tu namuunga mkono Mhe. Freeman Mbowe kuelekea kwenye uchaguzi wa viongozi wa chama chetu.

"Hatua za kinidhamu zilizochukuliwa hazijafuata utaratibu kulingana na katiba ya chama chetu, wanapaswa kuniingiza kwenye kamati ya maadili kwa tuhuma zinazonikabili, sijatukana kiongozi yeyote bali ni maoni tu niliyotoa mtandaoni”
amesema Ntobi.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2023 Ntobi aliwahi kusimamishwa Uenyekiti wake kwa mwaka mmoja kutokana na makosa ya kinidhamu.

Ntobi hivi karibuni maekuwa akilalamikiwa kwa baadhi ya maandiko na kauli zake dhidi ya Mgombea wa Uenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu

View attachment 3196896
Ntobi hana nidhamu.Ni kibaka.Ajirekebishe.
 
Kwahiyo Lissu Ana Nguvu Kuliko Mbowe Kwenye Chama...
 
Back
Top Bottom