Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Timu ya Taifa ya Uganda 'The Cranes' imejiimarisha kileleni kwenye kundi L katika michuano ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2019, nchi Cameroon baada ya kuichapa Lesotho mabao 3-0 kwenye uwanja wa Namboole mjini Kampala Uganda.
Uganda Cranes, wamefikisha alama saba baada ya mechi tatu, wakifuatiwa na Cape Verde yenye alama nne huku Tanzania na Lesotho wakiwa na alama mbili.
Ukurasa wa mabao ulifunguliwa na Emmanuel Okwi anayekipiga kunako timu ya Simba SC ya Tanzania katika dakika ya 11 kabla ya mchezaji Farouk Miya wa NHK ya Croatia kuandika bao dakika ya 36.
Ukurasa ulifungwa kama ulivyofunguliwa na yule yule Emmanuel Okwi kwa bao safi la kichwa katika dakika ya 63 ya mchezo.
Timu hizo zitarudiana jumanne Oktoba 16 kwenye uwanja wa Setsoto mjini Maseru, siku ambayo Tanzania 'Taifa Stars' akivaana na Cape Verde uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.