Iko maeneo ya Sanawari karibia na mahakama ya Mwanzo Enaboishu kando kando ya mto Themi.Ehhh, hii shule naikumbuka wakati nipo TCA na kina marehemu Method Mogella. Tulikuwa hata kwenye michezo hatukutani kwani mlikuwa watoto wadogo saana kimichezo. Hivi ilikuwa mitaa gani pale Arusha? Nilikuwa naisikia tu. Ilboru wakajinyua wakaja pale chuoni tukawachapa goli hadi wakaona aibu.
Hata hivyo nawasifu kwa ujasiri wa kuja kucheza na sisi.
ulichosema kina usahihi husiopingika ila kwa sasa shule imebadilika nafikiri baada ya Advanced Level kuanzishwa walioko Ordinary Level wamekuwa wanapata changamoto kubwa kusoma na kuondoa ile aibu ya kupata division four zisizohesabika. Pia kitendo cha kufanya mchujo wakati wa kuingia kidato cha tatu na nne umesaidia wanafunzi kufanya vizuri kwenye mitihani yao.Sipo (au Upo...)
acha utani.. hivi unafikiria zile div isiokuwa namba ya kuhesabia (sifuri) zilivyokuwa nyingi unafikiria mwisho wake ni nini...
mie mwaka wangu '83. div 1 = 2, div 2 < 10 (i blv 7), div 3 < 22 (nafikiri ni namba sahihi), div 4 sikumbuki (plenty) na div 0 > 40 kati ya (mkondo a-d) wanafunzi 152 tuliofanya mtihani wa baraza.
Mhe kweli wewe wa long time pale kama kipindi hicho ndio yalikuwa yanajengwa mabweni ya wasichana. Unastahili shikamoo kutoka kwangu "SHIKAMOO"class of '80-'83. mmmh! hebu nikumbuke jinsi lile zogo la foleni za kande (lunch) pale jikoni na mzee 'kijicho' na fimbo kuhakikisha hakuna anaerudia au kula 'anti-log' kupata kande.... ooops nimesahau na ile kazi ya kubeba mawe toka mtoni hadi mabweni (ya wasichana) wakati huo ndio yalikuwa yanajengwa.
Waauh!! Nice eperience from ScorpioMama, hawa wote sijawakuta pale kipindi nilichosoma ila nimependa kujua haya yote please tuendelee kukumbushana mengi kuhusu shule yetu hii yaliyopita ni dhahabu jamatupo! 1987 - 1989 bwenini tukiwa matron bibi, mzee mashauri! mwal ndossi mchungaji sasa natumai, mwal Letara,
Eti Mganga wa Jadi, how do you feel now? Unaweza kumshauri mwanao au mdogo wako aende kutuliza kiu kwa style ambayo ulikuwa unatumia wewe? Do you think its conducive? Nahitaji majibu yako pindi ukipita hapa ili tuache kuwapotosha wadogo na watoto wetuNawakumbuka mademu wazuri wa Enaboishu, wakati tunatoroka Ilboru kwenda kutuliza kiu kidogo baada ya kupiga book kali kwa mzee Kitemango.
ulichosema kina usahihi husiopingika ila kwa sasa shule imebadilika nafikiri baada ya Advanced Level kuanzishwa walioko Ordinary Level wamekuwa wanapata changamoto kubwa kusoma na kuondoa ile aibu ya kupata division four zisizohesabika. Pia kitendo cha kufanya mchujo wakati wa kuingia kidato cha tatu na nne umesaidia wanafunzi kufanya vizuri kwenye mitihani yao.
Ila nilitegemea kuwa wanafunzi wengi wa Enaboishu wangejitokeza kuchangia mada hii lakini naona wamejitokeza wachache sana na wengine ni kutoka shule na vyuo vingine.
Mkuu nashukuru kama nawe ni mmoja wapo, wangejitokeza wengi ingekuwa safi sana.Mkuu Sipo
wanafunzi wa Enaboishu tuko wengi sana hapa jamvini sema wengi hawataki kujitokeza kwasababu wanazozijua wenyewe.
Juzi nilikutana na Mwl Letara siku hizi ni mchungaji wa KKKT anatesa na L/Cruiser Hard top ya kanisa.Mwl Mbaga ni Financial manager Leopard Tours,Mwl Losaro ni Mwl mkuu wa Kimandolu secondary na Mwl Okonkwo (mwl wa Kiingereza)sikumbuki jina lake halisi ni marehemu.
Wanafunzi wengi wa Enaboishu wa miaka yetu wameshatangulia mbele ya haki hasa wale waliokimbilia Mbuguni mara baada ya kumaliza shule na wengi hawakungoja hata kumaliza shule.
MWENYENZI MUNGU azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. AmenWanafunzi wengi wa Enaboishu wa miaka yetu wameshatangulia mbele ya haki hasa wale waliokimbilia Mbuguni mara baada ya kumaliza shule na wengi hawakungoja hata kumaliza shule.
hili la wanafunzi wengi wa shule mkoani Arusha kukimbilia migodini hasa uko Mbughuni (Mererani) ndio tatizo kubwa sana na linapelekea wengi kutokumaliza elimu zao kwenye ngazi tofauti. Ila nafikiri sasa hali itakuwa imebadilika ingawa nina muda sijafuatilia kuhusu suala hiliwaliokimbilia Mbuguni mara baada ya kumaliza shule na wengi hawakungoja hata kumaliza shule.
hili la wanafunzi wengi wa shule mkoani Arusha kukimbilia migodini hasa uko Mbughuni (Mererani) ndio tatizo kubwa sana na linapelekea wengi kutokumaliza elimu zao kwenye ngazi tofauti. Ila nafikiri sasa hali itakuwa imebadilika ingawa nina muda sijafuatilia kuhusu suala hili
Mkuu wachimbaji wa kigeni kwa kiasi fulani wamewafukuza wachimbaji wa asili kwenye machimbo ya Mererani maarufu kama Mbughuni kwa mkoani Arusha. Lakini ukienda Arusha na kuwauliza vijana wengi kuhusiana na Mererani watawalalamikia sana AFGEM kuwa wamewaharibia maisha yao kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwabana na hata kuwasababishia ulemavu wa kudumu pale wanapohisiwa au kugundulika kuwa wametoka na madini kwenye migodi. Lakini cha ajabu huwa wanawashangaa hata polisi wetu ambao wamekuwa hawachukui action yoyote kutokana na either kuhongwa au masuala mengine ya influence kutoka kwa viongzi wa juu wenye mahusiano na viongozi wa AFGEM. Kipindi cha nyuma vijana wa Arusha walikuwa na maisha mazuri sana kabla ya hili wimbi la uwekezaji na wawekezaji.Hali ya migodi Mererani si nzuri kwa sasa madini yanapatikana kwa shida sana.Makampuni ya wazungu ndiyo yameweza kubakia katika biashara.Wamasaai nao wameshakiambia Mererani wamejaa tele maeneo ya Arusha by night (St Thomas) .Wazawa siku hizi hawachimbi mawe wamebaki madalali.Biashara ya udalali imetawaliwa na wamasai na wajaluo siku hizi.