Jamiitrailer
Senior Member
- Oct 20, 2019
- 190
- 452
Habari wakuu,
Huu mzozo wa kibiashara kati ya Malawi,Afrika ya Kusini na Tanzania sidhani kama ungekuwepo kama Jumuiya ya SADC ingekuwa inafanya kazi zake sawasawa kwa mantiki ya kusimamia utekelezaji wa maazimio yake.
Nasema hivi kwa sababu nchi zote hizi tatu katika mgogoro ni wanachama wa SADC.
Izingatiwe kwamba mwaka 2008 nchi zote wanachama za Jumuiya SADC,jumuiya ya COMESA na jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) walikubalina na kisha kusaini makubaliano kuanzisha ushirikiano wa kibiashara kwa hizo jumuiya tatu...TRIPARTITE FREE TRADE AREA (TFTA)...,eneo huru kibiashara baina ya nchi wanachama kwa mantiki ya kupunguza ushuru(tariff) katika bidhaa zinazotembea baina ya nchi zao.
Lengo likiwa ni kuondoa vikwazo vya kibiashara ili kuwarahisishia watu wao kufanya biashara kiwepesi ili kupunguza umaskini.
Hizo jumuiya tatu zina jumla ya nchi wanachama 26.
Kila jumuiya inawajibu kuangalia na kusimamia wanachama wake kama endapo wanatekeleza au kukiuka maazimia na malengo ya TFTA. Kwa vile huo mzozo wa kibiashara wahusika wake ni wanachama wa SADC,ilikuwa ni jukumu la SADC kutafuta kiini na kutatua mzozo.
Ni jukumu la SADC kimuuliza mwanachama wake Afrika ya kusini kwa nini anazuia ndizi tola Tanzania zisiingie soko lake. Pengine maelezo ya utetezi ya Afrika ya kusini yangetupa picha bora endapo wao ndo msingi wa tatizo au pengine tatizo lipo upande wa Tanzania yenyewe.
Ikumbukwe kwamba hata kukiwa na eneo huru la kibiashara,bado vegezo na masharti vinatakiwa kuzingatiwa linapokuja suala la ubora wa bidhaa inayoingia.
Hata waziri wa kilimo,Bashe alitakiwa kuwa wazi zaidi kwetu na kutueleza ni sababu zipi zilizofanya Afrika ya kusini izuie ndizi toka Tanzania lakini ikubali ndizi toka Msumbiji.
Kwa upande wa Malawi, wao uamuzi wao ni TOTAL BAN,....marufuku kwa bidhaa zote za kilimo toka Tanzania.
SADC ilitakiwa kuwahoji vikali Malawi kwa nini wameamua kuchukua uamuzi waliouchukua. Jibu la Malawi likiwa ni kulinda soko la bidhaa za kilimo za ndani, ..basi tayari watakua wamevunja makubaliano ya SADC na TFTA...na namna ya kumkabili kiadhabu inajulikana....ikiwezekana kuondolewa uanachama.
Ukiwa mwanachama unapata ahueni ya kiwango cha kodi kinachofanana kwa aina fulani ya bidhaa kwa nchi zote wanachama. Katika makubaliano ya TFTA,nchi wanachama zilikuwa huru kupanga kiwango cha kodi walichokitaka kwa bidhaa toka kwa nchi ambazo siyo wanachama.
Nimewahi kuandika hapa jukwaani namna jumuiya ya SADC ilivyo na utendaji wa kizimamoto kwa kufanya maamuzi kisiasa zaidi kuliko kuchukua maamuzi kulingana na hali halisi.. nikitolea mfano uamuzi wa watendaji wa SADC kukiuka n kupuuzia maelekezo ya wataalam wa kijeshi wa SADC na badala yake kupeleka kikosi cha watu 1200 tu,..tena chenye silaha nyepesi kana kwamba wanaenda kulinda amani tu,na siyo kuingia vitani kuikabili M23 yenye kikosi cha Rwanda na silaha za kisasa...huku wanajeshi wawili wa SADC toka Afrika kusini wakiwa wajawazito.
Pengine SADC ni kioo cha namna ya serikali ya nchi wanachama zinavyoendeshwa,....hazina umakini.
Inawezekana vipi nchi iingie makubaliano kisha ikiuke na kusifanyike chochote. Ndo maana nchi zetu bado ni maskini.