Nitarudia tena na tena kusema kwamba hakuna sababu za msingi ambazo tunaweza kujenga hoja ya kumwondoa Kikwete kama mgombea wa CCM na kumweka mtu mwingine. Hakuna mtu mwingine yeyote ndani ya CCM anayefaa kusimama uchaguzi wa mwaka 2010 kama sababu kubwa tunazojenga ni zitahusiana na Maslahi ya Taifa..
Kwanza kabisa nashindwa sana kuelewa kwa nini tunawalaumu viongozi ambao wanatekeleza sera za chama, hata kama ni kinyume cha matakwa ya wananchi. Nitawakumbusha tena kwamba Mwinyi aliyeteuliwa na Nyerere alikuwa kiongozi kwa mihula miwili pamoja na kwamba aliharibu na uchumi wetu kudodorora bado wananchi tulimchagua Mkapa, mgombea toka chama kilichoshindwa kutusogeza hata hatua moja mbele..
Haya alipoingia Mkapa tulijenga matumaini vile vile lakini akatuacha mataani awamu ya pili, yet bado wananchi tukamchagua Kikwete tena kwa asilimia 80 baada ya chama chake kuboronga Uchumi wetu kwa miaka mitano... Sasa tulitegemea nini hasa Kikwete angeweza kukifanya nje ya sera za chama chake ambazo zimetufikisha hapa tulipo.. Na tunapowachagua watu hawa huwa tuna send message gani kwao?..hakuna zaidi ya kwamba wananchi wanaridhika na Utawala uliopo hivyo Kikwete hawezi kufanya tofauti na kile mlichoridhika nacho kwa miaka 40 iliyopita.
Hatuwezi kumlaumu dereva wa gari kwa kuchelewa kufika trunakokusudia ikiwa tatizo ni utaratibu na ratiba ya shirika la gari hilo ni kusimama kila kituo na kuchukua abiria wengine.. Mtabadilisha kkila dereva lakini kama utaratibu bado ni ule ule sidhani kama mnamtendea haki Kikwete kwa sababu ni nyie wananchi mlomchagua mkijua fika kwamba Mkapa na uongozi wa CCM waliharibu Uchumi wa nchi hii, leo mnataka Kikwete afanye kinyume.. Na nina hakika akifanya hivyo atakuwa Dikteta kwa sababu safari ya CCM ni kutupeleka Tunduma na yeye anahakikisha tunaelekea Tunduma hata kama matakwa yetu wananchi ni kwenda Moshi.. mwenye makosa hapa ni nani?.. na kibaya zaidi gari lilipofika Morogoro tumeisha pita Chalinze watu mnataka Kikwete ageuze gari kurudi njia ya Moshi kinyume cha waajiri wake na wale wote waliomchagua kwa kura asilimia 80 kuwafikisha Tunduma.
Hutaki kwenda Tunduma, panda bus jingine, swala sii dereva jamani hata Mtikila anaweza kuwafikisha Moshi pamoja na kwamba gari lake bovu, at least linaweza wafikisha njia panda Korogwe..Lakini kwa ujinga wetu siosi wenyewe tunaendelea kupanda bus la kwenda kusini tukitegemea somehow pengine tunaweza fika Moshi kwa sababu dereva huyu kijana ana lugha nzuri, bus zuri na kadhalika..
Ukweli utabakia kwamba Kikwete anafanya yote mazuri kulingana na malengo ya chama chake. Ameongeza hesabu za majengo ya shule, barabara zinajengwa, misaada inaongezeka, Ajira nchini zimeongezeka, umaarufu wa Tanzania unazidi (Asha Rose Migiro yuko UN), Mabangusilo wanaanikwa, Vyama vya Upinzani wanapoteza watu muhimu kuhamia CCM. Viongozi wanaoiba wazi wazi wanaachishwa kazi bila kufikisha mahakamani ili kulinda Usalama wa Taifa..Lengo la Tanzania kuwa na Mabillionea 100 karibu inakamilika.. Nini zaidi mnataka?..
Kikwete ktk kampeni zake hakuwaahidi kupambana na Mafisadi, hakuwaahidi kurudisha nyumba za serikali, hakuwaahidi jambo lolote ambalo serikali yake haifanyi kazi na record zote zinaonyesha ongezeko la utenda kazi ktk kila sekta alizowaahidi pamoja na kwamba hazijakamilika...Safari ni kwenda Tunduma na anahakikisha mtafika Tunduma.. Can't U people get it?..Hutaki kwenda Tunduma shuka, toka ktk bus hilo kabla halijakufikisha mbali kwani hizi lawama za kumlaumu dereva haziwezi kukusaidia kitu. Nasema tena Hakuna kiongozi yeyote CCM ambaye atapigana na Ufisadi at the level mnayoitaka, hakuna! kwa sababu kila mmoja wao ana scandal kubwa inayomhusu.. Wewe na mimi hatuifahamu na KULINDANA ndio ILANI ya kwanza ya chama CCM...
People have invested time and money kuhakikisha chama kinakwenda Tunduma, wewe mlalahoi huwezi kubadilisha kitu zaidi ya kutopanda bus hilo. Period!